Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii, Musoma

Mradi wa ujenzi wa Gati mpya ya Mwalo wa Musoma unaojengwa na Mamlaka ya bandari ,umefikia  katika hatua za mwisho na wakazi wa eneo hilo wameanza kuutumia kwa ajili ya shughuli za kibiashara.

Akizungumza  na Waandishi was Habari mapema leo Mkoani Mara katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya Maendeleo iliyopo katika bandari za Ziwa Victoria, Mhandisi wa TPA,Abraham Msina amesema ujenzi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni605 .

"Mradi huu ambao ulianza tangu Novemba 2018 na kukamilika Mwaka huu May chini ya kampuni ya Kitanzania ambayo inaitwa Pentel  utaweza kuongeza mapato kwa mamlaka ya bandari na kurahisisha usafiri kwa wakzi wa eneo la Musoma"

Mhandisi Msina amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa Sana kwa Jamii kwani  lengo ni kusaidia upakiaji wa abiria na boti ndogo za mizigo na uvuvi.

Ametaja kuwa hapo awali Wakazi wa la Musoma walikuwa wakipaki vyombo vyao kando tu lakini kwa sasa Kila mtu anaweza kupaki chombo kwa usalama
 Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari katika Ziwa Victoria , Abraham Msina akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa gati ya Mwalo wa Musoma mkoani mara
 Moja ya boti zinazopaki katika Gati Mpya ya Mwalo wa Musoma katika mkoa wa Mara ikipakia mizigo katika bandari hiyo iliyojengwa kwa gaharama ya Milioni 605
 Mmoja wa Wakazi wa Musoma David Katikilo akieleza faida zilizopatikana mara baada ya kukamilika kwa mradi huo wa Bandar
 Mhandisi Mjenzi akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa TPA Hatua zilizobakki katika kukamilisha mradi huo wa ujenzi wa bandari mpya ya Mwaloni
Gati ya Mwaloni  Musoma Mkoani Mara inavyoonekana kwa juu mara baada ya kukamilika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...