Na.Vero Ignatus,Arusha

Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala ili kuinua vipato vyao na kupunguza tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi hususan waliohitimu elimu katika vyuo mbali mbali.

Akizungumza katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya utengenezaji wa mifuko hivyo pamoja na mafunzo ,Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation Neema Robert amesema kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo ili kuongeza idadi ya wazalishaji wa vifungashio hivyo na kupelekea bei kuwa rafiki kwa wananchi kutokana na uzalishaji kuongezeka.

Kwa upande wao Vijana waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza mifuko iliyotolewa kwa njia ya vitendo zaidi Rosemary Shedrack amesema kuwa kwa sasa wameanza kutengeneza mifuko na kuisambaza katika masokombalimbali pamoja na kujipatia fedha zinazowasaidia kujikimu na kujiendeleza kimaisha.

Mary Daudi ni moja kati ya vijana wanaotumia fursa hiyo amewataka vijana wengine kuiga mfano na kutumia fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani vifungashio hivyo vinahitajika kwa wingi nchini baada ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...