Vodacom Tanzania Foundation imezindua ripoti ya maendeleo ya jamii na mkakati mpya wa kuchochea ukuaji jumuishi leo Juni 27, 2019 ikiwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ambayo imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo na leo imezindua ripoti yake ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika tukio lililopewa jina la "Alama za upendo wa Vodacom" na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Afya(TAMISEMI), Josephat Kandege, maafisa kutoka washirika wa maendeleo na wadau wa kitaifa na kimataifa imeelezwa kuwa.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika tukio lililopewa jina la "Alama za upendo wa Vodacom" na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Afya(TAMISEMI), Josephat Kandege, maafisa kutoka washirika wa maendeleo na wadau wa kitaifa na kimataifa imeelezwa kuwa.
Taasisi ya Vodacom Foundation imewekeza zaidi ya shilingu bilioni 11 katika miradi ya jamii ambayo imedhamiria kuboresha maisha ya watu takribani milioni 3 nchini kupitia miradi mbalimbali hususani afya ya uzazi, elimu na huduma jumuishi za kifedha.
Akizungumza katika hafla hiyo Kandege amepongeza jitihada za Vodacom Tanzania Foundation katika kusaidia jamii na kusisitiza ushirikiano kati ya wadau mbalimbali.
"Nawapongeza sana Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha maisha ya watanzania na hasa katika sekta ya afya ya uzazi, elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Kuendeleza Tanzania ni jukumu letu sote hivyo basi ni muhimu sana tuungane pamoja kutimiza azma hii ya taifa letu. Natumai kwamba ripoti hii itatuhamasisha sote kuchangia Nguvu katika kuboresha maisha ya watanzania" ameeleza Kandege.
Aidha Kandege amesema kuwa ni jambo jema kwa makampuni ya namna hiyo kuiga mfano wa kampuni Vodacom kwa kushiriki katika kusaidia jamii katika masuala ya kijamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi amezungumzia juu ya mkakati huo mpya wa Taasisi hiyo na kueleza kuwa,
"Mkakati wetu wa 2019-2021 umezingatia mipango ya maendeleo ya nchi (Tanzania) na malengo endelevu ya maendeleo (SDGs) huku tukilenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha, ubora wa elimu na kuchochea mabadiliko katika sekta ya kilimo. Kama mtandao wa simu unaoongoza nchini, tuna nafasi ya pekee kuchangia maendeleo ya jamii na ya kiuchumi nchini kwa kupitia matumizi ya teknolojia ya simu." Ameeleza.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kampuni za simu zina fursa kubwa na wajibu wa kutumia teknolojia na uvumbuzi wa kidijitali kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza ufanisi wa watu. Kampuni ya Vodacom imekuwa ikifanya hivyo tangu mwaka 2000.
Pia Mkurugenzi wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Rosalynn Mworia, amesisitiza mashirika kuwekeza katika miradi inayolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
"Tumeshirikisha wadau mbalimbali katika uzinduzi wa ripoti hii ili kuwahamasisha kuwekeza katika miradi ya kuboresha jamii na kuchochea ushirikiano zaidi baina yetu na wao ili kufikia lengo la kuwa taifa lenye maendeleo jumuishi.” amesema Rosalynn.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali, imechangia vilivyo katika kuboresha maisha ya Watanzania kupunguza umasikini, kuboresha elimu, kuwezesha Wanawake na Wasichana, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Afya (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege( wa pili kulia) akizindua ripoti ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Afya (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege( wa pili kulia) akifurahi mara baada ya kuzindua ripoti ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Afya (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege( wa pili kulia) akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa uzinduzi ripoti ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi akisoma hotuba iliyokuwa inahusu Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation wakati wa uzinduzi ripoti ya Taasisi hiyo ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe akizungumza kuhusu mamlaka hiyo inavyofanya kazi bega kwa bega na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation wakati wa uzinduzi ripoti ya Taasisi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meza kuu
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka taasisi mbalimbali za hapa nchi wakiwa kwenye uzinduzi ripoti ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi ripoti ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation ya mchango wa maendeleo ya jamii kwa miaka mitatu iliyopita (2014-2017) pamoja na mkakati mpya wa miaka mitatu 2019-2021 unaolenga kuchochea elimu jumuishi, ukuaji wa sekta ya kilimo, kuboresha mazingiza na ujumuishwaji wa watu kwenye mifumo rasmi ya kifedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...