Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla akisalimiana na Sheikh Othman Zuberi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kitengo cha Biashara cha kampuni ya Vodacom Tanzania kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Arjun Dhilon
Waziri wa maliasili na utalii, Hamis Kigwangalla (Katikati)akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam.

Waziri wa maliasili na utalii, Hamis Kigwangalla (Katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi (Kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni hiyo katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...