Editha Edward-Tabora 

Wafanya biashara wilayani Nzega mjini Mkoani Tabora wamelalamikia mwingiliano wa kimamlaka wa ukusanyajj wa ushuru wa  huduma  kati ya Halmashauri ya wilaya ya Nzega na mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) ambayo yamekuwa yakiwaathiri  kibiashara wilayani humo 

Yamesemwa hayo katika kikao kilichoitishwa na meneja wa mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA)  mkoa wa Tabora Thomas  Masese  ambacho alikiitisha kwa ajili ya kupokea ushauri na kero kutoka kwa Wafanyabiashara wa wilayani humo wakaitumia fursa hiyo kulalamikia mwingiliano wa ukusanyaji wa ushuru baina ya Halmashauri ya mji na TRA

Baadhi ya Wafanyabiashara hao akiwemo self Haruna wametaka kujua ni nani mwenye dhamana ya kukusanya ushuru kati ya   TRA  na Halmashauri ya mji na kwa viwango gani vya malipo na kwa biashara zipi ambazo wanapaswa kulipia ili kuondoa mkanganyiko huo

Katika kikao hicho Wafanyabiashara hao wameiomba TRA kuongeza timu ya Maafisa ili kuharakisha kutembelea biashara na kutoa ukadiliaji wa ulipaji wa kodi pamoja na kuhimiza kampuni iliyopewa jukumu la kusambaza Mashine za EFD toka mwaka juzi kupeleka Mashine hizo

Akijibu malalamiko hayo meneja wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Tabora Thomas Masese amebainisha  utofauti wa ukusanyaji wa ushuru kati ya taasisi yake na Halmashauri kwa kuchukua asilimia kutoka kwa Wafanyabiashara na kuwa ahidi Wafanyabiashara hao kukutana na Mkurugenzi ili kuweza kuondoa usumbufu huo.
Pichani ni Meneja wa TRA Tabora  Thomas Masese akizungumza na Wafanyabiashara katika kikao kilichofanyika mjini Nzega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...