NA  Andrew Chale,Kibaha Pwani.

WALIMU wa mchezo wampira wa Wavu nchini wamepata mafunzo ya mchezo huo kutoka kwa Mkufunzi wa Kimataifa kutoka shirika la mpira wa Wavu Duniani (FIVB), Tony Westman.

Mafunzo hayo ya wiki mbili yamekutanisha walimu na wakufunzi wa mchezo huo wakiwemo kutoka Visiwani na Zanzibar na Tanzania Bara.

Katibu Mkuu wa Mpira wa wavu Nchini (TAVA) Alfred Seliengia amesema mafunzo hayo yataleta motisha kutokana na mbinu na masuala ta kiufundi.

"Mafunzo ya wiki mbili. Kwa vitendo na baadae daradani. Kutoka Tanzania Bara 21 na Visiwani Zanzibar wao wapo Nane. Kati yao Wanawake wapo Sita na Wanaume 23" amebainisha Katibu huyo.

Aidha ameongeza kuwa kati yao hao Walimu 15 na Walimu wa michezo wengine kutoka vilabu na timu mbalimbali.

Nae mkufunzi huyo wa Kimataifa, Tonny Westman amesema Tanzania inaweza kupiga hatua kwenye mpira wa wavu kama misingi itawekwa mapema kwa walimu na wanafunzi wanaopenda mchezo huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa makocha wa mpira wa Wavu nchini, Dismass Dickiamili amewashukuru TOC kwa ufadhili wa kozi hiyo ambayo ni 'leval one International ' ambapo itasaidia wavu kufika mbali.

"Mafunzo haya yanaendeshwa kwa mwaka wa tatu sasa chini ya ufadhili wa TOC". amesema Dick.Katika mafunzo hayo. Mwalimu huyo ameweza kutoa mbinu mbalimbali za mchezo wa wavu na namna ya kuweza kuzitumia kwa lengo la kukuza wavu nchini.

Nao baadhi ya wanaopatiwa mafunzo hayo wamebainisha kuwa mafunzo ni mazuri hivyo yatawajenga na pia kusaidia wengine ili kuendeleza wavu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...