WANANCHI wameaswa kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ambao wanakuwa na nia njema ya kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja bila ya kuwa na ubaguzi wa rangi kabila au dini.
Kadhalika wananchi wametakiwa kudumisha upedo na mshikamano miongonimwao bila kubaguana kwani ndio njia pekee ya kudumisha ushirikiano ambao hautaweza kuwagawanya au kuwatenga kwa itikadi na imani zao.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya monaban Trading and Farming ya jijini hapa,Dkt.Philemon Mollel,aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika baraza la Eid el Fitr,lililofanyika jana katika Taasisi ya Zawiyatul Qadiriyyat iliyopo Ngarenaro jijini hapa.
“Ndugu wakae pamoja kwa amani na upendo pia wakumbuke kuwasaidia watu wenye mahitaji maluum katika jamii wakiwemo asikini,yatima,wajane na wazee wasijiweza kwani wao hawakupenda kuwa katika hali hiyo”alisema mollel.
Alikemea baadhi ya tabia ambayo wamekuwa nayo baadhi ya watu kwa kuwa na dharau na kuwanyanyapaa watu hao na kuwataka kutowatenga na kushirikiana nao kwa hali na mali na kuacha kuwatenga kwani wao ni binadamu kama walivyo wengine.
Katika baraza hilo la Eid,Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Monaban Trading and Company limited,Dkt.Philemon Mollel,alichangia lori kumi
za mawe na fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kingo ya mto ngarenaro ambao umekuwa ukileta adha kubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Twarika,Mkoani hapa,Abdi Omar Bin
Said,alisema kuwa taasisi yake imejikita zaidi katika utunzaji wa mazingira na kuhakikisha kuwa wanadhibiti kingo za mto ngarenaro kwa
kupanda miti zoezi ambalo wamekwisha lianza.
Amengeza kuwa kadhalika Taasisi hiyo pia imejikita katika kutoa elimu katika fani mbalimbali kwa lengo la kuwafanya vijana kupata elimu na ujuzi wa kuweza kujiajiri ikiwa ni pamoja na kulea watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo mpaka sasa wana vituo vitano.
Kwa upande wake mlezi wa taasisi hiyo hapa nchini,Salum Darwesh,alilisitiza umoja na upendo miongoni mwa madhehebu yote ya
dini na kusema kuwa ili mtu akamilike katika kutimiza majukumu yake ya kwa jamii ni lazim awe na vitu vitatu ambavyo ni afya njema na utu.
“Ukiwa na afya njema utaweza kusimama na kutembea popote,ukiwa na kitu ni rahisi kusema chochote na kutoa msaada kwa wahitaji na endapo una utu utawajali wenzako kuwathamini na kuwapenda"alisema Darwesh.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...