NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WANANCHI wanaopisha miradi mikubwa ya umeme ,katika mikoa ya Pwani ,Dar es Salaam na Dodoma watarajie kulipwa fidia zao wakati wowote baada ya uhakiki kukamilika.
Zoezi hilo limechukua kipindi kirefu kutokana na uhakiki hivyo fedha hizo zisingeweza kutolewa haraka kwani wapo waliokuwa wakitaka kujinufaisha kupitia malipo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Vitendo huko Kibaha wakati alipokuwa akizindua uwashaji umeme,alitaja maeneo hayo kuwa ni njia za Rufiji Chalinze,Dar es Salaam - Chalinze na Chalinze hadi Dodoma .
Alieleza, wanatarajia kukutana na wananchi wanaohusika na jambo hilo,na hakuna wa kunyimwa haki yake . "Tunaomba samahani kwa kuchelewesha fidia kwani tunajua baadhi wanasubiri tangu mwaka 2013 lakini kulihitajika umakini ili kuepuka upigaji,"
"Tanesco sasa nao watakuwa na miradi ya kuunganisha umeme kwa maeneo ulikopita umeme mkubwa ili kila mtu apate huduma ya umeme," alifafanua Subira.Nae mwakilishi wa meneja wa Tanesco mkoa wa Pwani ,Kenneth Boimanda alisema, nyumba zote wataalamu watapita kukagua eneo lote la mradi ili umeme uweze kuwafikia wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alisema ,wakandarasi wahakikishe wanawafikia wananchi wote ili kuondoa malalamiko.Koka alibainisha, wananchi wanajukumu la kulinda miundombinu ya umeme ili isihujumiwe au kuibiwa kwani serikali inatumia gharama kubwa kuijenga.
Awali akisoma risala ya mtaa huo wa Vitendo ,mtendaji Juma Hamis alisema kuwa kati ya nyumba 620 zilizopatiwa umeme ni 20.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...