GARI aina ya Coaster iliyokuwa imebeba wasanii ambao wapo kwenye msafara Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy imepata ajali eneo la Mikumi mkoani Morogoro.
Hata hivyo inaelezwa hadi sasa hakuna aliyepoteza maisha kutokana na ajali hiyo ila baadhi ya wasanii wamepata majeraha.Ajali hiyo imetokea mapema leo katika eneo hilo na inaelezwa wasanii hao walikuwa wanaelekea Sumbawanga.
Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ya mkononi, Meneja wa Msanii Nandy amesema ni kweli kuna ajali imetokea na wao wamepata taarifa na kwa sasa wanafuatilia na kisha watatoa taarifa kamili.
"Tumepata taarifa kuwa Coaster iliyokuwa imebeba wasanii imepata ajali eneo la Mikumi.Kwa sasa tunafuatili ili kujua kinachoendelea na hali za watu wetu na baada ya hapo ndio tutakuwa na taarifa rasmi ya kueleza kuhusua ajali hiyo"amesema Meneja huyo.
Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika ingawa baadhi ya mashuhuda wanadai eneo hilo kulikuwa a gari aina ya roli iliyokuwa imeharibika barabarani.
Hivyo dereva wa Coaster wakati anataka kuipita akaona kuna gari nyingine inakuja mbele yake na wakati anataka kukwepa ndipo akapoteza muelekeo.
Hata hivyo inaelezwa Nandy hakuwa kwenye gari iliopata ajali hiyo kwani alikuwa kwenye gari nyingine lakini naye alikuwepo eneo ambalo Coaster hiyo imepata ajali.Michuzi Blog itaendelea kukupa taarifa zaidi ya kinachoendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...