SERIKALI
Imeishukuru Benki ya NMB kuendelea kusaidia katika Sekta ya Elimu kwa
kuchangia madawati baadhi ya Shule zilizo na upungufu na uhitaji mkubwa
wa madawati ili wanafunzi waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea madawati 50 yenye thamani ya Sh, milioni 5 kutoka Benki ya NMB, mgeni rasmi Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, aliyemwakilisha Mkurugnezi, aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuchangia madawati kwa shule zilizo na upungufu.
Aidha alisema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hiyo ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono juhudi za serikali inayotilia mkazo suala zima la masomo ili kila mtoto aweze kupata elimu.
''Pamoja na Serikali kutangaza kuwa elimu ni bure ili watoto wetu wote waweze kwenda shule, lakini bado inahitahi kushirikiana na wadau wa Elimu kama Benki hii ya NMB ii iweze kufikia lengo la kila mtoto kwenda shule,
Mwaka jana 2018 watoto wa darasa la kwanza walioandikishwa walikuwa ni 22, 000 lakini kwa mwaka huu wameongezeka na kufikia 38,000 hii inaonyesha kuwa hata wazazi wameamka ka kuelewa lengo la Serikali kutoa elimu bure, na idadi hii namini itazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na mwamko wa wazazi''. Alisema Tabu
Naye Meneja wa NMB Tawi la Gongolamboto, Rehema Mwibura, alisema kuwa katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Sekta ya Elimu na Afya, NMB itaendelea kuwa karibu na Jamii kwa kutoa sehemu ya faida yao kusaidia Sekta hizo zenye uhitaji.
''Pamoja na kwamba tumeshatoa misaada ya aina hiio kwa shule mbalimbali nchini na vituo vya afya lakini bado tutaendelea kurudisha faida tunayoiapata kwa jamii kwa kuchangia katika masuala ya kijamii. NMB imekuwa ikichangia sekta za Elimu na Afya kwa kutoa vifaa mbalimbali kama vitanda vya Hospitali na vifaa tiba na Madawati pamoja na viti vyake kwa shule za Msingi na Sekondari.

Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (wa pili
kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa Madawati 50 yenye
thamani ya Sh. milioni 5 kutoka kwa Meneja wa Tawi la Gongolamboto,
Rehema Mwibura (kushoto) na Meneja Mahusiano Biashara za Serikali wa
NMB, Faraja Kaziulaya (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya
madawati hayo kwa ajili ya Shule ya Msingi Yangeyange iliyopo Msongola
Manispaa ya Ilala, jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...