Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa umeme

 Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la Kufua umeme na watatumia fursa ya bwawa hilo kwa kuangalia namna ya kujenga mtambo na kuanza kuzalisha maji kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi.


 Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es salaam (DAWASA) wameweza kuwa moja ya chachu ya mradi wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji (Stiegler's Gorge) kwa Kukarabati mradi wa maji uliojengwa miaka ya 1970.

Mradi huo wa maji ni kwa ajili ya kutoa huduma katika kambi ya ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa Rufiji Mkoani Pwani ambao utakamilika Juni 2022 na kuzalisha megawati 2,115 baada ya kujenga miundo mbinu ya maji.

DAWASA wameweza kufanikisha hilo kwa kujenga mfumo wa maji kutoka kwenye chanzo cha Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) na kulaza mabomba yaliyopeleka maji kwenye matanki.

Mradi huo wa kufua umeme umewekewa jiwe la msingi na Rais Dkt John Pombe Magufuli jana  ambapo kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa uchumi.

Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo zimefanyika kando ya eneo litakapojengwa bwawa la maji na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nishati wa Misri Mhe. Dkt. Mohamed Shaker, Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Tanzania, Wabunge, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali.

Kwa upande wa DAWASA, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema watatumia fursa ya bwawa hilo kwa kuangalia namna ya kujenga mtambo na kuanza kuzalisha maji kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi.

Amesema, lengo la DAWASA ni kuleta maji kutoka maporomoko ya Stieglers Gorge na  mchakato huo tayari umeanza ikiwemo kuunda timu ya wahandisi wa mradi kufanya usanifu ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wake huku fedha zitakazotumika zikiwa ni za ndani na utekelezaji wa mradi huo mkubwa utasaidia kuondoa ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani na kuifanya Dar es Salaam kuwa salama zaidi kwa matumizi ya maji safi na salama.

Mradi wa maji kutoka  maporomoko ya Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) umesimamiwa na DAWASA na kugharimu kiasi cha Milioni 604.9 na umekamilika Mwezi Agosti mwaka jana  ukiwa na uwezo  kuzalisha maji lita 209,000( laki mbili na elfu tisa) kwa ajili ya matumizi ya kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji  wa megawati 2115.

Mradi huo wa maji utawasaidia wakandarasi kuwa na miundo mbinu wezeshi itakayowapatia maji muda wote wa matumizi yao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanusi mkubwa na kusaidia mradi wa ujenzi la bwawa la kufua umeme kukamilika kwa wakati.

DAWASA walikarabati  miundo mbinu iliyokuwa chakavu ikiwemo ukarabati wa eneo la chanzo pamoja na ufungaji wa pampu moja mpya itakayokuwa na uwezo wa kuchota maji mtoni kiasi cha lita 2.41 kwa sekunde, ulazaji wa mabomba ya kusambazia maji  na urefu wa Km 1463 kutoka mahali maji yanapopatikana ambapo  mradi huo wa maji utapeleka maji kwenye  matanki makubwa mawili.

Katika ukarabati huo pia waliweza kuhusisha bomba la kusafirishia maji (GS pipe) kipenyo cha nchi 3, ujenzi wa bomba jipya la plastic(HDPE) la kusafirishia majighafi kutoka mto Rufiji hafi kwenye tanki na kituo cha kusafisha maji, ukarabati wa kituo cha kusafisha maji, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji, ujenzi wa bomba la kusafirishia maji, ukarabati wa matanki mawili ya zamani ya lita 12,500 na 22,500 na ufungaji wa dira za maji , air valve 4 na gate valve 4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...