Na.Khadija Seif, Michuzi tv

AMBER rutty na Mumewe wote peponi,Salam akikuchukia huvuki boda, ni miongoni mwa vionjo vinavyopatikana kwenye wimbo mpya wa Mkali wa Muziki wa Singeli nchini Abdallah Omari a.k.a Dulla Makabila unaoitwa "Waongo" akitoa ujumbe kwa Mashabiki kuwa kuna stori zingine ni uongo tu waache imani potofu.

Makabila ni Msanii ambae amekuwa akifanya vyema kwa upande wa Muziki huo kwa sasa nchini.Pia ameweka wazi sababu zinazomfanya Muziki wake usishuke kiwango kwa Mashabiki zake na uendelee kuishi.

Makabila amesema zipo sababu nyingi ila kuwa kwake nadhifu hasa kwenye swala la Mavazi kumeendelea kumpatia maadili mengi likiwemo la mmoja wa wasanii waliochaguliwa kutumbuiza kwenye Tamasha la Wasafi Muleba mwaka huu linalotarajiwa kufanyika julai 19 mwaka huu.

"Wasanii wengi wa Singeli hawajipendi,wachafu wanavaa Mavazi ya kihunihuni ndio sababu hata wadau ,taasisi na waandaaji wa Matamasha imekua ngumu kuwaita wafanye kazi nao ,"

Pia ameeleza kuwa kwa sasa yeye ndio Mkali na mfalme wa Muziki wa Singeli kutokana na utofauti wake na Muziki wake na waimbaji wengine wa Singeli.

"Asilimia kubwa wanaimba mashairi ya matusi ambayo my hawezi kusikiliza Muziki ambao ujumbe wake sio mzuri na hauna maana ila Mimi nimebobea kwenye kuburudisha na kuelimisha kama wimbo wangu mpya unaoitwa "Waongo" ambao nimejaribu kufafanua zaidi kuhusu watu wenye imani potofu kuhusu vitu mbalimbali kuwa waache imani hizo,"

Pia ametoa shukrani kwa Msanii wa Muziki wa kufokafoka (HIP HOP) country boy kutokana na kushirikiana nae bega kwa bega katika kuboresha kazi zake za kisanaa hasa upande wa Mavazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...