Na Mwandishi Wetu, Pwani

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani imepongeza hatua ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni Brela(BRELA) kutoa mafunzo kuhusu usajili wa biashara zao kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Abdalla Ndauka alisema leo mkoani hapa kuwa mafunzo yamewasaidia namna ya kujua kusajili majina ya biashara nembo za biashara jambo ambalo litawasaidia Katika kuzalisha na kudhibiti wezi wa Brand za biashara zao vilevile watafuata sheria za nchi kwa kuzingatia usajili huo.

Hata hivyo Ndauka amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhakika wa upatikanaji wa mtandao katika baadhi maeneo baadhi yao kutokujua matumizi ya kompyuta hivyo alishauri mafunzo yawe endelevu ili wote wanufaike na elimu iliyotolewa.

Kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika mafunzo hayo wilayani Mkuranga na Kibaha Mkoani Pwani Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Mketto amesema mafunzo hayo yamewashirikisha wafanyabiashara, wanasheria, maafisa biashara pamoja na wajasiriamali wilayani Mkuranga na Kibaha Mkoani Pwani.

Katika kujua umuhimu wa matumizi ya mfumo huo kujisajili kwa njia ya mtandao kwakuwa sasa imerahisishwa ukilinganisha na ya zamani kwa njia ya makabrasha.Amesema mafunzo hayo yamelenga kurahisisha 

usajili na kuondoa changamoto zilizokuwepo ambapo mtu anaweza kujisajili popote alipo ambapo wanasheria maafisa biashara walionufaika na mafunzo hayo katika kila Halmashauri watawaelimisha wafanyabiashara wengine katika maeneo yao.Amesema wanasajili kampuni yenye mtaji kuanzia 20,000 hadi milioni moja ambapo makampuni 149,929 yamesajiliwa kabla ya mfumo na baada ya mfumo majina ya biashara 456,152.

Ametaja baadhi ya changamoto kwenye mfumo huo kuwa ni pamoja na kutokuwa rafiki na wafanyabiashara,uhitaji wa vitambulisho vya utaifa na mawasiliano kutokuwa mazuri.

""Wengi wa wafanyabiashara hawana vitambulisho vya Taifa inawawia vigumu kumudu mfumo huu licha ya mfumo kuongeza idadi kubwa ya usajili wa makampuni ukilinganisha na mfumo wa zamani kwa njia ya makabrasha,"amesema.

Mketto pia amewakumbusha wadau umuhimu wa kulipia mizania ya mwaka kwa upande wa makampuni na ada kwa upand we wa wafayabiashara kwani ni muhimu kwa kuwa baadhi hulimbikiza madeni mwisho wa siku inawawia vigumu kulipa kutokana na malimbikizo ya madeni.

"Mwisho wa siku inakuwa maumivu kwa taasisi sisi sio taasisi kazi yetu kutoa huduma kwa wadau lipieni mizania kwa wakati ukichelewesha unalimbikiza faini inaongezeka,"amesema Mketto.Kwa upande wa makampuni yaliyojisajili muda mrefu kwa dhumuni fulani Mketto aliyataka yakishindwa kujiendesha wasifunge biashara badala yake wajiridhishe kila mwaka wanalipia kwani ipo siku itawafaa katika biashara zao kuingia katika zabuni zenye ushindani Kwa vile kampuni zao zitakuwa hai.

Hata hivyo wafanyabiashara wa MKuranga wameelezea ugumu wa kusajili kupitia mfumo huo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtandao ktk maeneo wanayoishi na upatikanaji wa vitambulisho vya taifa.Dk Judicate Ndosi Ndengerio alisema mafunzo yamepanua wigo wa uelewa kwa upande wao lakini changamoto zifanyiwe Kazi.

Kwa mujibu kwa kujibu wa Mketto ni kwamba mafunzo hayo yamefanyika mikoa yote kupitia kanda ikiwa ni pamoja nyanda za juu kusini,kati,kaskazini,magharibi na kumalizia mkoa wa Pwani zoezi ambalo ni Endelevu litafanyika mikoa yote ili kuwarahisishia wafanyabiashara kutembea umbali mrefu kufanya usajili wa makampuni ama leseni za viwanda.
 Meneja wa Utawala na Fedha Bw. Bakari Mketto akitoa somo kwa maafisa biashara wanasheria wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani katika mafunzo yaliyohusu Usajili wa Biashara na makampuni kwa njia ya mtandao ambayo Tanganyika mjini Kibaha katika ukumbi wa mikutano jengo la ofisi za mkuu wa Mkoa huo.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maofisa wa Brela hawapo pichani katika ukumbi WA mikutano jengo la ofisi za Mkuu wa Mkoa huo wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...