Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)kupitia chuo cha Mafunzo ya kijeshi TMA kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha , kimetiliana saini mkataba wa pili wa Makubaliano ya kutoa Mafunzo ya Elimu ya Shahada ya Sayansi ya kijeshi na chuo cha uhasibu (IAA) cha jijini Arusha yatakayofanyika kwa miaka Mitatu.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mikataba ya Makubalino Mbele ya Waandishi wa habari ambayo yamefanyika katika chuo hicho ,mkuu wa chuo cha Uhasibu ,Njiro prof,Eliamani Sedoyeka amesema kuwa ushirikiano huo kati ya TMA na IAA ni malengo ya muda mrefu katika kuongeza ubora wa elimu kwa jeshi ili kwendana na sera ya serikali kuweza kufikia malengo ya uchumi wa viwanda hapa nchini
Alisema mkataba wa kwanza wa uashirikiano ulisainiwa desemba mwaka 2015 na Novemba 20,2017 walizindua rasimi shahada ya sayansi ya Kijeshi(Bachelor of Military Science).
Aidha amesema kuwa hadi sasa shahada hiyo ina jumla ya wanafunzi, wanajeshi wapatao 208 wanaosoma chuoni hapo huku akiahidi chuo hicho kuwapatia elimu iliyo bora kwa maendeleo ya nchi na kuhakikisha jeshi la wananchi linapata elimu bora inayoendana na mtizamo wa rais John Magufuli katika ukuaji wa technolojia na hatimaye kujenga jeshi lenye nguvu
"Ushirikiano huu umekiweka chuo katika hali nzuri na kwamba na tunaahidi kutoa elimu bora kwa jeshi letu na pia kuongeza Nyanja nyingine za ushirikiano zaidi na vyuo vingine" Amesema Frof.Sedoyeka
Alisema Chuo cha uhasibu Arusha,Kinatoa kozi mbalimbali kwa ngaIbza cheti,Stashahada(Diploma),Shahada (Degree), Shahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) na shahada ya Uzamili(Masters) katika maaomo UA Uhasibu, Manunuzi na Ugavi,Benki na Fedha ,Uchumi,Uwekezaji,Biashara,Sayansi ya Kompyuta na teknolojia ya Habari.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) ,Brigedia Jenerali ,Stephen Mnkande amekishukuru chuo cha uhasibu Arusha kwa ushirikiano mkubwa waliyouonyesha kwa kuwa amelenga kuandaa mahusiano mazuri baina ya jeshi hilo na chuo cha uhasibu katika nyanja ya Elimu ya juu.
Makubaliano hayo yanahitinisha mchakato wa makubaliano hayo ambayo tayari yamesasainiwa tangu Julai 9 mwaka huu 2019 na kwamba tukio hilo lilizikutanisha tasisi hizo mbili chuo cha kijeshi ,Monduli na chuo cha uhasibu Njiro kwa lengo la kudumisha mahusiano kwa mustakabari wa mahusiano mapana ya Taifa la Tanzania.
Picha ikionyesha mkuu wa chuo cha Uhasibu ,Njiro prof,Eliamani Sedoyeka pamoja na mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) ,Brigedia Jenerali ,Stephen Mnkande wakikabidhiana mikataba waliosaini hafla fupi ya makabidhiano ya mikataba ya Makubalino hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...