Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe Salama.
Kiongozi wa Mila ,Mzee wilson Kaaya,Mshili mkuu ukoo wa Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama
Mhe.Diwani kata ya Akheri (wa kwanza kulia) Viongozi wa Dini na Mila wakati wa uzinduzi
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt.Maneno Focus akizungumza kwenye kikao hicho.

Kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama imezinduliwa katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru ambapo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro, amesema Wilaya hiyo itasimamia vyema Kampeni hiyo inayolenga kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, hivyo jamii na watoa huduma za afya wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa wakati 

"kuwa mjamzito  na kujifungua si ugonjwa hivyo kinamama na watoto ni lazima wawe salama kwani uhai ni haki yao"amesisitiza Mhe Muro.

Aidha Muro amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus Kuwakumbusha watoa huduma za afya kutekeleza wajibu wao kwa weledi pia kutumia lugha zenye staa na rafiki kwa wagonjwa sambamba na kuacha matumizi ya simu za mkononi yasio muhimu wakati wa saa za kazi "kauli nzuri kwa mgonjwa humpa faraja na kuwa sehemu ya tiba" amefafanu Muro.
Mganga Mkuu Dkt.Maneno Focus amesema Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ambapo kwa Halmashauri hiyo hali ya uwepo wa dawa muhimu wakati wa kujifungua ni zaidi ya asilimia 98.
Aidha  Dkt. Focus  aliainisha kuwa katika kipindi cha mwezi January hadi Juni mwaka 2019 kumekua na vifo  viwili vitokanavyo na uzazi ingawa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi toka kwenye jamii ambao hawafiki kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo kampeni hiyo inalenga kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa dini, siasa, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha  vifo vya uzazi vinadhibitiwa.
Naye Mratibu wa Kampeni hiyo ngazi ya Halmashauri Ndg.Sikudhani Mkama amesema Halmashauri imeweka mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama inafanikiwa na ametoa rai kwa  jamii na familia kutimiza wajibu wao ili kupunguza na kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Afya Philomena Marijan toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW ambalo huwawezesha vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi pamoja na kuongeza ushiriki wao katika ma swala ya afya ya uzazi,uchumi na uongozi, ameipongeza Halmashauri hiyo  kulipa kipau mbele swala la afya ya vijana na elimu juu ya afya ya uzazi.
Aidha uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri umekamilika kwa maafisa Tarafa  kula kiapo cha usimamizi wa utekeleza wa Kampeni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...