Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAJUMBE wa kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,Mkoa w Arusha kimemchagua Gerad Munisi kuwa Katibu Mwenezi wa mkoa huo kujaza nafasi hiyo iliyokuwa wazi kutokana na aliyekuwa Katibu Uenezi Shaban Mdoe kuteuliwa kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Ushindi huo haukuwa rahisi ilibidi kuingia awamu ya pili kutokana na awamu ya kwanza mshindi kutokuvuka nusu ya kura .Ambapo awamu ya Kwanza Gerad Munisi alipata Kura 26 ,Bakari Rahib Msangi alipata kura 21 na Elipokea Urio alipata kura 7

Katika awamu ya Pili Gerad Munisi alizoa kura 33 na Bakari Rahm Msangi alipata kura 19 na Ndipo msimamizi wa Uchaguzi huo Katibu wa ccm mkoa wa Arusha, Mussa Matoroka, alipomtanga Gerad Munisi kuwa mshindi baada ya kuvuka nusu ya kura .

Akitoa Nasaha zake Munisi, ameahidi utumishi uliotukuka na pia atashirikiana na kila mmoja kwa ajili ya kazi za chama .Amesema siku za hivi karibuni kumekuwa kukitolewa taarifa za upotoshaji na vyama vya upinzani kutokana na miradi inayotekelezwa na serikali maeneo mbalimbali ambapo wanakuwa wakidai wao ndio wameileta jambo ambalo sio la kweli.

Akiahirisha uchaguzi msimamizi wa uchaguzi Mussa Matoroka, amewasisitiza wajumbe kuhakikisha wanasimama kidete kuhakikisha wananchi wanajitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika hivi karibuni nchini kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...