Na Marco Maduhu na Suleiman Abeid - Malunde1 blog

Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiongozwa na madiwani wa CCM wamemkataa mkurugenzi wa manispaa hiyo, Geofrey Mwangulubi kwa madai ya kushindwa kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa kila mara na madiwani hao hivyo.

Madiwani hao wamedai tabia ya mkurugenzi kushindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa katika vikao huenda ikawachonganisha na wapiga kura wao kutokana na kutokuwepo kwa miradi yoyote ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao. 

Hali hiyo imejitokeza leo Jumatatu Julai 29, 2019 katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wakati madiwani hao wakithibitisha agenda zilizopangwa kujadiliwa ambapo diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila (CCM) alisimama na kuzikataa ajenda hizo na kisha kutoa hoja yake ya kutokuwa na imani na mkurugenzi Mwangulumbi. 

Hoja ya diwani Nkulila iliungwa mkono na baadhi ya madiwani ambapo hata hivyo, Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Shinyanga (Serikali za mitaa),Alphonce Kasanyi , na mwanasheria wa manispaa hiyo, Doris Dario walisimama na kuwataka madiwani kusitisha maamuzi yao kwa vile yanapingana na utaratibu. 

Kasanyi alisema madiwani walipaswa waitishe kikao maalumu cha kutokuwa na imani na mkurugenzi pamoja na kumwandikia barua mkuu wa mkoa kuhusu kumkataa mkurugenzi huyo. 

Hata hivyo, ushauri wa Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga,Alphonce Kasanyi na mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga, Doris Dario haukusikilizwa na madiwani na badala yake baadhi yao walisimama na kuchambua kwa kina baadhi ya maagizo yaliyowahi kutolewa na baraza la madiwani na mkurugenzi kushindwa kuyatekeleza kitendo ambacho walidai ni dharau na hawatakuwa tayari kuendelea kufanya naye kazi.

Diwani wa viti maalumu, Shella Mshendate alisema hawako tayari kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi anayeitwa Geoffrey Mwangulumbi na kitendo chao hakimaanishi kuvunja baraza bali hawamtaki mtu, na siyo mkurugenzi ambapo alimuomba Naibu Meya atafute mtaalamu mwingine akae kwenye kiti cha mkurugenzi na kikao kiendelee.

Naye diwani wa kata Kambarage ,Hassan Mwendapole (CCM) naye aliunga hoja ya kutokuwa na imani na mkurugenzi huyo kutokana na kushindwa kutekeleza maazimio yao hali inayofanya madiwani kutokuwa na miradi ya maendeleo kwenye kata zao hivyo kuonekana kutoa ahadi kwa wananchi ambao ni wapiga kura wao. 

Diwani wa kata ya Kizumbi Ruben Kitinya (CCM) alisema hawezi kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi huyo kwani yale wanayojadili kwenye baraza na kamati mbalimbali hayatekelezwi hivyo hana imani na mkurugenzi huyo. 

Pamoja na vitisho vya kuvunjwa baraza na kufanyika kwa uchaguzi mpya vilivyotolewa na mwakilishi wa katibu tawala msaidizi, kwamba kitendo chao cha kumkataa mkurugenzi kinamaanisha kuvunjwa kwa baraza, bado madiwani walisimama na msimamo wao wa kumkataa mkurugenzi ambapo walivua majoho na kutoka nje ya kikao. 

Kwa upande, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi amesema hivi sasa hawezi kuzungumza chochote kuhusu maamuzi hayo ya madiwani hao ya kutokuwa na imani naye hivyo anasubiri maamuzi kutoka ngazi za juu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Diwani wa kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi( CHADEMA) ambaye alishasimamishwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani kutokana na tabia ya kukosoa utendaji kazi wa mkurugenzi huyo,amewapongeza madiwani wa manispaa hiyo kwa kumkataa mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulubi akisoma ajenda za kikao cha baraza la madiwani,kabla baraza la madiwani halijavunjika - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Madiwani wakipitia ajenda za kikao kabla ya kuvunjika kwa kikao cha baraza la madiwani.
Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao kabla hakijavunjika 
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alizikataa agendaza kikao na kisha kutoa hoja yake ya kutokuwa na imani na mkurugenzi Mwangulumbi. 
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akivua joho kutoka nje kutokana na kutokukubaliana na ajenda za kikao. 
Diwani wa Viti Maalumu,Maria Nyangaka akiwa amevua joho kuunga mkono hoja ya madiwani kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Diwani wa kata Kambarage ,Hassan Mwendapole (CCM) akiunga hoja ya kutokuwa na imani na mkurugenzi huyo kutokana na kushindwa kutekeleza maazimio yao hali inayofanya madiwani kutokuwa na miradi ya maendeleo kwenye kata zao hivyo kuonekana kutoa ahadi kwa wananchi ambao ni wapiga kura wao. 
Diwani wa kata ya Kizumbi Ruben Kitinya (CCM) akiunga hoja. Alisema hawezi kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi huyo kwani yale wanayojadili kwenye baraza na kamati mbalimbali hayatekelezwi hivyo hana imani na mkurugenzi huyo. 
Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Shinyanga (Serikali za mitaa),Alphonce Kasanyi akizungumza ambapo alisema madiwani walipaswa waitishe kikao maalumu cha kutokuwa na imani na mkurugenzi pamoja na kumwandikia barua mkuu wa mkoa kuhusu kumkataa mkurugenzi huyo. 
Mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Doris Dario akiwataka madiwani kusitisha maamuzi yao kwa vile yanapingana na utaratibu. 
Madiwani wakitoka ukumbini baada ya kikao cha baraza la madiwani kuvunjika. 
Madiwani wakitoka ukumbini. 
Madiwani wakitoka ukumbini 
Madiwani wakitoka ukumbini .Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...