Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeaanda mafunzo ya Siku mbili kwa  wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi kuhusu upendeleo wa makundi maalumu kwenye sheria ya ununuzi wa umma.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye amesema serikali imeweka kifungu maalumu kinachozitaka taasisi nunuzi kutenga asilimia 30 ya ya bajeti zao za manunuzi kwenda kwa wanawake, Vijana,wazee na watu wenye ulemavu.

Bilabaye amesema, sheria hiyo inalenga kuwaandaa vijana ambao hawana ajira, wajiweke kwenye Makundi maalumu ili kujipatia kazi za ununuzi kutoka kwenye taasisi za umma.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi, Wajumbe wa bodi za zabuni na taasisi za umma zilizotajwa na sheria (Special Group Supporting Entity) ili kuzijengea uwezo wanamna bora ya kuyaandaa makundi maalumu ili yaweze kushiriki kwenye zabuni.
 Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma ( PPAA), Hamis Tika  akitoa mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yanayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa PSPTB. Kulia ni Afisa Mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa PSPTB, Shamim Mdee.
 Baadhi ya washiriki wakichangia mada kwenye mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

 Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi, Wajumbe wa bodi za zabuni na taasisi za umma wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya PSPTB baada ya kuhitimisha siku ya kwanza ya mafunzo hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...