Na Mwandishi Wetu,Tunduru

SERIKALI mkoani Ruvuma, imepiga marufuku taasisi za fedha ambazo hazijasaliwa na zinawakopesha walimu na watumishi wengine wa Umma katika mkoa huo, kuacha mara moja kuchukua vitambulisho na kadi za benki kama dhamana.

Kwani taasisi hizo zinakwenda kinyume na mifumo ya ukopeshaji, na zina wadhalilisha sana walimu na kupelekea baadhi yao kuhaathirika kisaikolojia na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa huo Christina Mndeme, alipokuwa anaongea na walimu wa shule za msingi na sekondari na waratibu Elimu kata, wakati wa hafla ya kuwapongeza Walimu wa mkoa huo kufuatia na matokeo mazuri katika mitihani ya darasa la saba 2018 na kidato cha sita 2019.

Pia,amewaasa Walimu kuishi kwa maadili mema na kujiepusha na madeni kupita kiasi na kwa kuwa tabia hiyo inawafanya washindwe kufundisha watoto madarasani.

“taasisi za fedha zilizopo mitaani ziache kuchukua kadi za benki na vitambulisho vya watumishi, tabia hii sitaki kusikia katika mkoa wangu kwani inawadhalilisha na kuwaibia watumishi,siko tayari kuona walimu wanaendelea kuumia”alisema Mndeme.

Sambamba na hilo amewashauri walimu wasiwe wapesi wa kutoa kadi za benki na kutokubali kuingia katika mikataba ambayo haina masilahi kwa familia.

Alisema, hawezi kuzui mwalimu kukopa fedha,lakini ni muhimu kutumia taasisi zinazo fuata sheria,kanuni na taratibu za nchi.
Amewataka walimu wakuu kuwa na ushirikiano mkubwa na walimu walio chini yao,kuwapenda na kuwa kama familia ili kutoathiri taaluma.

Aidha,amewapongeza Walimu wa wilaya ya Tunduru na mkoa mzima wa Ruvuma kwa kupandisha taaluma ya mkoa ambayo imepelekea mkoa huo kupata tuzo sita kwa shule za Msingi,kati ya tuzo hizo Halmashauri ya wilaya Tunduru imefanikiwa kupata tuzo nne.

Alisema, mafaniko hayo ni matokeo ya mshikamano mkubwa uliopo kati ya walimu wenyewe na viongozi wa wilaya ambao ndiyo wanao simamia sekta ya Elimu.

Kwa mujibu wa Mndeme,jitihada hizo si za kubeza kwani pamoja na upungufu mkubwa waWalimu lakini ukweli ni kwamba ufaulu unazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka na hiyo ni hatua madhubuti na makusudi ya wilaya ya Tunduru kuongeza ufaulu ili kufikia malengo ya Chama cha Mapinduzi ya kufaulisha kwa asilimia 90 ifikapo Mwaka 2020.

Alisema, Serikali imeendelea kuleta walimu ambapo jumla ya walimu 111 kati yao Walimu wa Sekondari 15 na Msingi 96 wamepelekwa katika wilaya ya Tunduru.

Amewaomba Walimu,waendelee kuchapa kazi na kuwapuuza wale wote wanao wakatisha tamaa kwa lengo la kuwavunja moyo.Kwa upande wake,katibu Tawala wa mkoa huo Profesa Rizik Shemdoe alisema,wilaya ya Tunduru imefanya vizuri katika skta ya Elimu kwa hiyo inastahili kupewa heshima kubwa.

Alisema, licha ya wilaya hiyo kuwa na idadi kubwa ya shule za Msingi,hata hivyo jambo la faraja kuona ndiyo wilaya yenye mafaniko makubwa katika mkoa huo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Awali Afisa Elimu msingi wa wilaya ya Tunduru Mwalongo alisema,katika matokeo ya kidato cha nne ufaulu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka wastani wa asilimia 76 hadi 100 ambapo shule 19 zilifanikiwa kuingia kuwa shule Bora Kitaifa.

Mwalongo alisema, kwa upande wa shule za msingi shule 54 zilifaulisha kwa asilimia 94 hadi 100 na mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kutoka kwa wadau wote wa sekta ya Elimu.

Pia alisema, mwaka 2019 Halmashauri kupitia idara ya Elimu imefanikiwa kulipa madeni yote ya walimu sambamba na kulipa stahiki zote za wastaafu kwa kipindi cha miezi sita pamoja na alimu 506 wamepandishwa madaraja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...