JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja MWAKILA S/O ALLY [32], mkazi wa Mwambene, Jijini Mbeya  kwa tuhuma za kupatikana na laini za simu [141] zenye usajili wa majina ya watu wengine.
Mnamo tarehe 12/07/2019 majira ya saa 13:00 mchana huko mtaa wa Itongo kata ya Mwambete tarafa ya Iyunga. Mtuhumiwa ambaye pia ni fundi umeme baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kumiliki laini hizo za simu 141 za mitandao tofauti zilizosajiliwa kwa majina tofauti ikiwemo “HALOTEL” laini 13, TIGO laini 29, TTCL laini 01, VODACOM laini 78 na AIRTEL laini 20. Pia alikutwa akiwa na vocha zilizotumika  za Vodacom 05, Tigo 04, Airtel 48, Halotel 03 pamoja na simu Itel 03, “Oking01 na “Hotwave01
Chanzo ni kujipatia kipato. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

AJALI YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU- WILAYA YA RUNGWE.
Mnano tarehe 14/07/2019 majira ya saa 09:00 huko Kanyegele kata ya kiwira tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe. Barabara ya kuu ya TUKUYU – MBEYA, Gari na. T. 359 DCA/T. 429 CMH Aina ya Howo mali ya kampuni ya “Overland” iliyopo “Dsm” ikiendeshwa na RAJAB S/O ISSA [40] ikiwa imebeba mafuta aina ya Petrol na Diesel kuelekea Tukuyu iliacha njia na kupindukia kolongoni na kusababisha uharibifu  wa mali na mafuta kumwagika baada ya “Tank” kupasuka. Aidha  msaidizi wa dereva aitwaye SALUMU S/O SAID[40] amepata majeraha. Chanzo cha ajali ni ubovu wa matairi ya gari hiyo.
Natoa wito kwa wananchi kutosogea maeneo ya ajali bila kuchukua tahadhari, kwani madhara ya kufanya hivyo ni kupata ulemavu wa viungo, au kupoteza maisha kutokana na hatari mbalimbali kama milipuko ya mafuta. 

AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO- WILAYA YA MBALIZI.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 20:30 u0siku, CHRISTINA D/O ANTHONY @ MWALINGO [37] aligongwa na gari huko katika Kata Inyala, Tarafa Tembela, Wilaya Kipolisi Mbalizi, Mkoa Mbeya, barabara ya Mbeya - Njombe na kusababisha kifo chake papohapo.  Gari na dereva hajafahamika. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Igawilo. Ufuatiliaji kumkamata dereva na gari unaendelea.

TUKIO LA MAUAJI -WILAYA YA MBEYA.
Mnamo tarehe 14.07.2019 majira ya saa 09:00 asubuhi huko meneo ya mtaa wa Mponja  Kata ya Igawilo, Tarafa Iyunga, Jijini Mbeya, mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la MARIA D/O FAUSTINE@KISANJI [22] Mkazi wa Mwanyanje alikutwa  amefariki dunia kwenye Pagala linalomilikiwa na mtu aitwaye ESTER D/O JOHN @MWANSHEMELA

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa mhudumu wa Bar itwayo SIKALAMANGA inayomilikiwa na DOMINICK S/O ABRAHAM.Ambapo mnamo tarehe 13/07/2019 majira ya saa 23:00 usiku marehemu aliondoka na  mtu asiyefahamika/jinsia ya kiume ambaye alikuwa anakunywa naye pombe. Kiini cha tukio ni ugomvi wa kimapenzi kati ya wawili hao. Msako mkali  unaendelea ili kubaini na kumkamata aliyehusika katika tukio hilo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu  na wahalifu kwa kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.
WITO:
Natoa wito kwa jamii kuacha, kujihusisha na vitendo vya kihalifu na kujishughulisha na kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato. Ni rai yangu kwa  wananchi/Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa katika barabara zenye miteremko mikali, na milimani kwani ajali nyingi hutokea maeneo hayo na kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

       Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...