Mgeni
rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo
juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo
Naimana.
Afisa
Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na
wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga
yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA)
iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna -
Kajunason/MMG, Morogoro.
Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI
(TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa
wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa
taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo.
Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
Kilima cha kisasa cha nyanya.
Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Watafiti
wa mazao ya kilimo nchini wametakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawafikia
wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijiji ili wakulima hao waweze
kulima kilimo chenye tija ikiwa ni katika kubabiliana na changamoto ya
ushindani wa masoko kitaifa na kimataifa.
Rai
hiyo imetolewa na Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba,
wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa
Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika
katika mjini Morogoro.
Bi. Chumba amesema kuwa watafiti hao endapo watafanya zao vyema zinaweza
kumkomboa mkulima na akaweza kupata soko bora la mazao yao na
itawakwambua kiuchumi.
"Niwashukuru
wataalamu maana nyie mmekuja wakomboa wakulima wadogo ambao mara nyingi
huwa ni ngumu kufikiwa matokeo yake wamekuwa wakilima kilima cha
mazoea ambacho hakina manufaa kwao," amesema.
Nae Meneja Miradi ya Taasisi ya TAHA, Bi. Elianchea Shanga amesema kuwa
kwa sasa wamesambaa mikoa mbali mbali ya Tanzania na lengo lao kubwa ni
kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha
tija.
"Sisi
lengo kubwa mkulima aone dhamani ya kile anachokilima maana tunasimamia
kuanzia kuandaa shamba, madawa na mbolea huku tukimpa ushauri na
kumtafutia soko," amesema.
Kwa upande wao wakulima Mwajuma Abdala wamefurahishwa na ujio wa Taasisi
ya TAHA huku wakielezea kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa mwiba kwao
kwa sasa ni mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea ukosefu wa
mvua huku wakiiomba serikali kuongezea nguvu katika kusaidia kilimo cha
umwagiliaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...