Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
CHAMA cha wafanyabiashara wa Madini Taifa (TAMIDA) kimelaani hatua ya vitendo vya utoroshwaji wa madini vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu jambo ambalo wameeleza ni uhujumu wa rasilimali za nchi na kuitaka serikali iwasake na kuwachukulia hatua kali ili kukomkesha matukio hayo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia tukio la hivi karibuni kukamatwa kwa madini mbalimbali yakiwemo Tanzanite yenye uzito wa kilogram zaidi 31 yaliyokuwa yakitoroshwa na wafanyabiashara kupitia mpaka wa Namanga ,kuelekea nchi jirani ya Kenya yakiwa yamefungwa kwenye viroba vya mchele.
Aidha Tamida imeishukuru Serikali kwa kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kuhamasisha wachimbaji kuuza madini yao katika masoko rasimi kwa kuwaondolea baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa na urasimu kwa wafanyabiashara wa madini nchini.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wa madini Taifa, Sammy Mollel (pichani)amesema kuwa Kuondolewa kwa tozo ya kodi ya zuio kwa asilimia 5 na kodi ya ongezeko la thamani asilimia 18 na tozo hiyo kutozwa asilimia 0 ni kuhamasisha biashara kufanyika katika mazingira rahisi.
Amesema kuwa Tamida na wachimbaji wa madini nchini wanalaani kwa nguvu zao zote na watatoa ushirikiano kwa serikali kwa wale wote wenye nia ya kutorosha rasilimali za madini kwa njia za magendo nje ya nchi wakati serikali imefanya mambo makubwa chini ya Rais Dkt.John Magufuli.
Ameeleza lengo la serikali ni kuondoa urasimu na kuhamasisha biashara ifanyike katika masoko rasimi na hivyo kuondoa ubaguzi na kudhibiti utoroshwaji wa rasilimali ya madini ili sekta hiyo iweze kutoa mchango wake katika pato la taifa na kukuza uchumi sisi tamida tunaunga mkono na kulaani utoroshwaji na hatua zichkuliwe kwa kuwasaka na kuwatia nguvuni.
“Hivyo basi tunaiomba serikali yetu ihakikishe inawasaka na kuwatia nguvuni wote waliohusika katika jaribio la utoroshaji wa madini hayo ili sheria ifuate mkondo wake na adhabu kali itolewe kwani wanaharibu taswira ya wafanyabiashara waaminifu”
Amesema wao kama Tamida watasimama na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kuona watanzania wananufaika na rasilimali za madini kwa kulipa mapato na kuzalisha kwa uwazi na utaratibu kwa sisi wafanyabiashara kufanya biashara kuwa wa wazi.
Akawataka wafanyabiashara kufuata utaratibu kwa kuongeza thamani ya madini na kuitaka serikali kuleta teknolojia ya kusanifu madini yetu ili wafanyabiashra waendelee kufanya biashara zao kwa uwazi kwani imeondoa urasimu mkubwa hivyo tunaishukuru serikali yetu kwa kutuandalia mazingira mazuri chini ya waziri Biteko.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...