Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO)mkoani hapa limewatahadharisha
wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu chini ya miundombinu
ya umeme ikiwemo transfoma,nguzo na nyaya,ikiwa ni pamoja na kukaa
mbali na maeneo ambayo matengenezo ya umeme yanafanyika.

Kadhalika Shirika hilo limewasihi wananchi kuhakikisha kuwa wanatumia wakandarasi wenye ujuzi na waliosajiliwa kufanya kazi za kuchora ramani na kutandaza nyaya za umeme pindi wanapohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme.

Afisa uhusiano wa Tanesco,Mkoani hapa,saidy mremi aliyasema hayo jana
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alipokuwa
akizungumzia tahadhari ya ajali za umeme kwa wananchi na mali zao.

Alisema kuwa wakati umefika kwa wananchi kutambua madhara makubwa
yanayoweza kujitokeza pindi wasipochukua tahadhari za ajali hizo za
umeme kwani licha ya kuharibu miundombinu ya umeme,pia hupelekea
wananchi kupoteza uhai pamoja na uharibifu wa mali.

“Nawasihi pia waendesha magari yanayobeba mizigo mikubwa na mirefu
wachukue tahadhari pindi wanapopita chini ya maeneo mbalimbali yenye
miundombinu ya umeme,pia wananchi wachukue taadhari kwa vitu
vilivyoguswa na nyaya za umeme zilizoanguka mfano miti,uzio na kamba
za kuanikia nguo”alisisitiza Mremi.

Afisa uhusiano huyo altumia fursa hiyo pia kuwasihi wananchi wanaotaka
kuunganishiwa umeme kufika moja kwa moja katika ofisi za Tanesco kwa
lengo la kuepukana na watu ambao wamekuwa wakijifanya maafisa wa
Tanesco(Vishoka)walioko huko mtaani ambao wamekuwa wakiwarubuni na
kuwatapeli.

Aliongeza kuwa fomu ya kuomba kuunganishiwa umeme hutolewa bure na
shirika hilo,na kwamba gharama za kuunganishiwa umeme zinajulikana
hivyo ni bora wananchi wakafika katika ofisi za shirika hilo zilizopo
katika Wilaya zote za mkoa wa Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...