Na.Khadija seif ,Michuzi tv

SHIRIKA la uwakala wa meli nchini (TASAC) limebainisha majukumu yake .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Emmanuel ndambo amesema shirika limepewa majukumu ya kusimamia na kudhibiti shughuli za usafiri wa majini kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na kutoa leseni kwa watoa huduma hizo.

"Kuhakikisha watoa huduma wanazingatia masharti ya uendeshaji pamoja na kulinda mazingira na usalama wa abiria na mizigo yao,"

Hata hivyo ndomba ameeleza kuwa kuna sheria ambazo zilitungwa na shirika hilo ikiwemo uwakala wa forodha na uondoshaji wa shehena kwa bidhaa Kama madini ,makinikia,mitambo,petroli,silaha,wanyama hai na nyaraka za serikali.

" majukumu mengine ni udhibiti wa nyaraka za mizigo,uhakiki wa mizigo inayoingia na kutoka pamoja na uwakala wa meli," alisema ndomba


Ndomba amebainisha maamuzi makuu mawili ambayo bodi ya wakurugenzi iliyoteuliwa iliunda ni pamoja na kuhakikisha shirika la uwakala wa meli (TASAC) inafanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kusimamia tozo zote zinazotozwa kwa wananchi .

Pia ametoa wito wakala wa forodha,pamoja na mawakala wote wa meli kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta ufanisi na kuboresha bandari zote.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la uwakala wa meli nchini (TASAC) Emmanuel Ndambo akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kutolea ufafanuzi sheria pamoja na majukumu yaliyoundwa na bodi hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...