Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limeufahamisha wadau na wananchi kwa ujumla kufahamu kwamba Bunge limepitisha sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imeleta mabadiliko katika sheria ya viwango namba mbili ya mwaka 2009.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TBS kupitia Mkurugenzi Mkuu wake Dk.Yusuf Ngeya amesema katika mabadiliko hayo TBS imeongezewa majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi, majukumu ambayo yalikuwa yanatakelezwa hapo awali na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA).

Amesema kuwa Wizara, taasisi na halmashauri zilizokuwa zimekasimiwa majukumu na TFDA kwa wakati huo kusimamia masuala ya usalama hasa katika machinjio ,bucha,mama lishe na mahoteli zitaendelea kufanya kazi hiyo wakati hatua za kuweka utaratibu mpya chibi ya TBS ukiendelea.


Pia Dk.Ngenya amesemawa kwa sasa matakwa ya kibali cha usajili wa bidhaa zinazoingizwa nchini,kilichokuwa kinatolewa na TFDA  na kuingizwa kwenye mifumo ya kieletroniki ya TRA kimeondolewa badala yake cheti cha ukaguzi TBS (CoC) au kibali cha shehena husika kinachotolewa na TBS kitatumika.

Pia wafanyabiashara hao leseni za biashara na usajili wa majengo ambazo zimekwisha muda wake, wataendelea kutoa huduma kwa katika kipindi cha mpito cha miezi mitatu wakati shirika likiendelea kukamilisha taratibu za uhuishaji wa vyeti husika .

"Vile vile wafanyabiashara ambao vibali vyao vimekisha muda wake  wafike katika ofisi za TBS iliyokaribu ama watume maombi kwa njia ya barua pepe ili kupatiwa barua itakayokuwa kielelezo katika kipindi cha mpito," amesema.

Pia amesema shirika linatoa hofu wadau wote kuwa wamba mabadiliko hayo hayataathiri utendaji wa taasisi kwani limejipanga vizuri kuhakikisha huduma hizo zinaendelea katika kiwango kinachotakiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana TBS, tunategemea kazi nzuri kutoka kwenu

    ReplyDelete
  2. Pamoja na kuaminiwa, naona hadi sasa TBS haijaweza kufikia kiwango cha utendaji cha TFDA. Ni kama tumerudi nyuma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...