Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imetoa tathmini ya ziara ya kikazi kutangaza na kutafuta masoko ya Utalii katika nchi za uchina na Korea ya kusini .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa bodi hiyo Jaji Thomas Mihayo amesema kuwa miongoni mwa matunda ya ziara hiyo ilikuwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya Touchroad international holding group ambayo imepanga kuleta watalii 10,000 kutoka China katika kipindi Cha mwaka 2019.

"Lengo kuu la ziara ya utangazaji Utalii ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaongeza sehemu ya umiliki wa soko kwenye solo la Utalii la China kwa kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania,fursa za uwekezaji zilizopo nchini na safari za ndege za ATCL kwenda China" Amesema Jaji Mihayo.

Katika ziara ya Korea ya kusini Jaji Mihayo Amesema kuwa walifanya mazungumzo na kampuni ya Utalii inayoongoza kwa kutoa watalii nje ya Korea ya kusini na kuzihamasisha kuleta watalii wao nchini Tanzania kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya Hanjin na HanaTour.

Jaji Mihayo ametaja kuwa walitumia fursa hiyo kuwaalika katika maonyesho ya Utalii yanayoandaliwa na TTB yajulikanayo kama Swahili international Tourism Expo(SITE) ambayo mwaka huu yatafanyika 20 Oktoba jijini Dar es Salaam na kampuni hizo zimekubali mwaliko.

Amesema Mkurugenzi wa kampuni ya shoestring travels ambayo inaongoza kwa Utalii wa upandaji milima Amesema kampuni yake ipo tayari kushirikiana na TTB katika kutangaza mlima Kilimanjaro na kuhamasisha watalii kutoka Korea kupanda mlima huu pamoja na kutangaza milima mingine Tanzania.

Alisema bodi ya Utalii Tanzania kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Korea ya kusini tunatarajia kuandaa ziara ya utangazaji Utalii (roadshow) ambapo wataweza tutaweza kukutana na kampuni nyingine zaidi za korea ya kusini .

Alimaliza kwa kusema katika ziara hiyo ya Korea ya kusini waliweza kufanikiwa kutembelea bustani ya Taifa ya Suncheon iliyopo katika mji wa Suncheon , na kukutana na uongozi wa bustani hiyo ambao umetoa eneo la umubwa was mita za mraba 1000 kwa ajili ya kutangaza Utalii katika bustani hiyo kwa kuanzisha bustani yenye taswira ya Tanzania.

Ametaja Tanzania ni Nchi ya Kwanza kwa bara la afrika kupata eneo katika bustani hiyo ambapo Nchi zingine zilizopata eneo hilo ni pamoja na Uholanzi, Mexico, Japan, Italia,Ufaransa, of China,Marekani, Uingereza na Uturuki.
Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji      Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi  kuhusua tathmini ya ziara ya China na Korea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...