Na Kijakazi Abdalla Maelezo
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa kuwepo kwa zoezi la
uchunguzi wa saratani ya kishingo ya kizazi ni kuweza kupata takwimu
sahihi ya kujua wanaosumbuliwa na maradhi hayo hapa Zanzibar.
Hayo ameyasema huko katika Hospitali ya Mnazi mmoja wakati akiangalia
zoezi zima la uchunguzi wa saratani wa shingo ya kizazi kwa wanawake.
Amesema kuwa kwa hivi sasa idadi kamili bado haijulikani kwa
wanaousumbuliwa na maradhi hayo jambo linaifanya kuweza kutoa takwimu
sahihi na hata maeneo gani yaliaathirika na maradhi hayo.
Aidha alisema kuwa kupata takwimu sahihi pia kutawezesha Wizara ya
Afya kuengeza bajeti ya tiba ili kuweza kurahisisha na kupambana na
maradhi hayo.
Aidha alisema kuwa maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi yanatibika
bila ya hata kwenda kwa waganga kwani tiba sahihi ya maradhi hayo
yanapatikana katika hospitalini.
Alisema kuwa kinamama walio wengi wamekuwa wanaamini kuwa ugonjwa huo
unatokana na kurogwa jambo ambalo sio sahihi hali ambayo inaweza
kutowafanya kutofika hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
“Kinamama wengi mnaamini maradhi haya yanatokana na kurogwa na hasa
wale wanawake wenye wakewenza kumbe sio sahihi”, alisema Waziri
Rashid.
Hata hivyo amewataka kinamama kujitokeza kwa wengi katika vituo vya
afya kuchunguza afya zao ili kuweza kujua hali zao mapema jambo ambapo
litaweza kuondokana na usumbufu mara wanapobainika wanasumbuliwa na
maradhi mbalimbali.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi
kupambana na maradhi mbalimbali hali kwa wananchi wake ili kuweza
kupata taifa lenye afya.
Nae Mratibu wa Mradi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi
kutokana Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China QI Xiaomin amesema kuwa
zoezi la kufanyia uchunguzi kinamama linafanyika kitaalamu kwa hali ya
juu kabisa.
Nae Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambikiza Zanzibar Omar Mwalimu
Omar amewataka kinamama kuitumia fursa iliyowepo ili kuweza kupatiwa
vipimo kwa uhakika.
Hata hivyo alisema uzuri wa kupatiwa vipimo kwa uhakika kutawezesha
kinamama kuondokana na kutumia gharama nyingi za matibabu pale
wanapobainika na maradhi kama hayo.
Nae Mwakilishi wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kaskazini Panya Ali
Abdalla ambae alishiriki katika zoezi la uchunguzi wa saratani ya
shingo ya kizazi ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja
na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuazisha zoezi hili .
Aidha aliwataka kinamama kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwani
halina malipo wala halina usumbufu kwa wale wanasumbuliwa na ugonjwa
huo na tiba yake inapatikana.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kulia ni Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.
Mmoja kati ya madaktari kutoka China Hupaohai akifanya uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Muakilishi Nafasi za Wanawake Panya Ali Abdalla akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanyiwa Uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed(katikati) na Naibu Waziri wa Afya kushoto yake wakiwa katika Picha ya pamoja na Madaktari Kutoka China waliofika Nchini kwa ajili ya kufanya Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake uliofanyika Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mmoja kati ya madaktari wanaoshirikiana na Madaktari
kutoka China Faiza Habibu (kushoto)akimfanyia mahojiano Mwananchi
Zuhura Bazi Mkaazi wa Chukwani katika uchunguzi wa maradhi ya Saratani
ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili
ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja
Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...