Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Multichoice nchini imeendesha usahili wa  pili wa  Kusaka vipaji kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 26 na wenye ndoto ya kuwa waongozaji wa filamu.

 Akizungumza na Michuzi tv Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice nchini  kupitia  King'amuzi Cha (DSTV)  Grace Mgaya amesema kuwa msimu huo ni wa pili na umeanza rasmi na vijana wanne (4) kutoka Tanzania ambao watakuwa miongoni mwa vijana 60 kutoka kote barani Afrika na hiyo ni  kupitia  Mpango wa umoja wa Afrika ambao unatafuta wabunifu 60 wa filamu na televisheni barani  Afrika na kuwaweka sehemu ya darasa la mwaka 2019.

"Vijana 60 kutoka kote barani Afrika ikiwemo Tanzania watapata fursa ya udhamini wa kujifunza uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni kwa mwaka mmoja katika awamu ya pili ya programu ya kusaka vipaji  vya waongozaji wa filamu Multichoice Talent Factory (MTF)," ameeleza.

Pia ameeleza kuwa fursa hiyo imezingatia vijana wenye uchu wa kuwa wabobezi watakaodhaminiwa kwa mafunzo hayo ya kitaalamu yanayoendeshwa  katika vituo vitatu barani Afrika ikiwa ni Nairobi, Lusaka na Lagos.

Aidha, Mgaya amefafanua kwa upande wa Tanzania, kuna nafasi nne za udhamini katika awamu hii ya pili ambapo  wanafunzi hao wataungana na wenzao kutoka Kenya,Uganda na Ethiopia katika kituo cha mafunzo cha Nairobi.

"Lengo la kuwanoa vijana wa kiafrika katika tasnia ya filamu ili kuwajengea uwezo, upeo,  ujuzi na weledi wa kiwango cha kimataifa katika uzalishaji na mapinduzi ya biashara ya filamu kwa ujumla. " ameeleza Mgaya.

Kwa upande wake Muongozaji bora wa filamu pamoja na picha jongefu nchini Adam Juma amesema ni wakati wa mapinduzi makubwa kwenye sekta ya filamu hapa nchini.

Juma amesema kuwa niaka miwili ijayo tutegemee mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Multichoice yataibua waongozaji wazuri na wanaofata mifumo mizuri ya uongozaji kutokana na tayari watakua wameshaiva kitaaluma.

 Pia ametoa wito kwa vijana watakaobahatika kuchaguliwa watumie fursa hiyo na watakaporejea nchini wasiache kuwashika mkono vijana wenzao ambao wanawiwa katika sekta ya filamu.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice nchini Grace Mgaya akitoa ufafanuzi kuhusu muitikio wa vijana waliojitokeza kwenye usahili wa pili wa Kusaka vipaji vya waongozaji wa filamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...