TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni Benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na binafsi ,pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi. Benki ina matawi 7 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha, Mbeya na Dodoma.
Kwa mamlaka iliyopewa Benki kuu imechukua uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Bw. Frank Nyabundege kuanzia tarehe 13 Julai 2019, kufuatia usitishwaji huo imemteua Bw. Fred Luvanda kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. Benki kuu ilichukua uamuzi huo chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2)(f)  pamoja na 33 (2)(b)cha sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006.
Ndugu waandishi wa habari, mkiwa na kazi kubwa ya kuhabarisha umma tunaomba muweze kutoa taarifa sahihi kuwa Benki ya TIB Corporate haiko chini ya usimamizi wa mabenki bali ni mabadiliko ya uongozi wa juu tu.              (Aliyeondolewa ni Mkurugenzi Mtendaji). Benki ya TIB Corporate inaendelea kuhudumia wateja wake kama kawaida kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.

Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla, wajue kuwa  huduma zinaendelea kama kawaida, pia mfahamu kuwa Serikali na Benki kuu inatambua umuhimu wa Benki hii hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha Benki  inazidi kuboresha huduma zake na kukua kwa maendeleo ya nchi yetu.
Niwaombe menejimenti pamoja na wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha benki inatimiza malengo yake.



Fred Luvanda

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...