Makamo wa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Vijana wa CCM Taifa *Ndg Tabia Mwita* amefungua mafunzo  Maalum kwa Wasichana kwa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mafunzo hayo Yaliyosimamiwa na kuratibiwa na *Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi *Ndg.Rose Robert Manumba* kwa Kushirikiana Taasisi ya Kijerumani FES kwa lengo la kuwaelimisha na kuwaongezea ujuzi na Maarifa yakiuongozi.

Pamoja na kufungua Mafunzo hayo Miongoni mwa waliyotoa na mada ni Ndg.Tabia Mwita na  amewasilisha Mada ya *Ushiriki wa wanawake katika siasa* ambavyo amesisitiza wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa bila kuogopa. Amewasihi wanawake kujiamini na kutokukubali kukatishwa tamaa. 

Makamu huyo  amesisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano ili kuendeleza kusaidia Serikali katika juhudi zinazofanyika kumuinua Mwanamke.

Aidha, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa *Rose Manumba* akiwa  amesisitiza kuwa ni muhimu sisi kama wasichana kuwa sehemu ya mabadiliko tunayotamani kuyaona katika nchi yetu na hata duniani kwa ujumla. Tuwe  tayari kutumikia nafasi zetu popote pale tulipo kuendelea kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dr. John pombe Magufuli anayepambana usiku na mchana kumuinua mwanamke wa kitanzania ili kuleta maendeleo katika Taifa letu. 

Wameshiriki wakufunzi mbalimbali kama Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation aliyewasilisha mada ya *Mchango wa asasi za kiraia katika kumuinua Mwanamke* Na Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digital aliyewasilisha mada ya;  *Namna gani msichana anaweza kuziona na kuzipata Fursa.* 

 *Ndg. Japhary Kubecha* ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya UVCCM Taifa katika kufunga mafunzo hayo amesisitiza wanawake kujituma katika kazi na sio kuridhika na nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kupata kwa kigezo kuwa ni wanawake.

Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali; Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni Lilian Rwebangira, Abdul-Rahman Killo na Mwanaidi ambao ni Maafisa kutoka UVCCM Makao Makuu.

Ndg Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Bi Tabia Mwita akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.

 Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa Ndg Rose Manumba na Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.



 Washiriki Mbalimbali wakifuatilia Mada 
 Sehemu ya Meza kuu ikiimba wimbo wa Hamasa Wapili kulia ni Ndg Tabia Mwita Makamu mwenyekiti wa UVCCM,Ndg Rose Manumba Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na Mratibu wa Mafunzo hayo(tatu kulia),(pili kushoto)Ndg Jafari kubecha mgamba (MNEC)anaewakilisha kundi la Vijana pamoja na wawasilishaji mada wakati wa Ufunguzi wa Semina elekezi ya kimkakati kwa Wasichana Mkoa wa Dar es Salaam.
 Ndg Rose Manumba akiongoza Mjadala kwa Washiriki

 Ndg Dorris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation akiwasilisha mada

 Suma Mwaitenda ambaye ni Mkurugenzi wa FURSA, kutokea Clouds Media Digita akiwasilisha mada
Ndg Jafari Kubecha Mgamba akizungumza wakati wa ufangaji wa Mafunzo maaalum kwa ajili ya wasichana wa mkoa wa dar es salaam (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI WA UVCCM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...