Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema VETA wamejipanga kwa kwenda kisasa katika kutatua changamoto zinazozunguka jamii.

Hayo aliyasema Biteko wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya  43 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema kuwa vijana wanaonyesha ujuzi pamoja na kuvumbua mambo mbalimbali.

Amesema kuwa VETA iende katika sekta ya Madini kwani kuna vitu vingi wanaweza kufanya.
Amesema kuwa kupata A katika mitihani sio sababu lazima mtu aonyeshe A hiyo ambapo VETA wanaonyesha uwezo wao kwa vitendo katika ugunduzi.

Nae Meneja Mawasiliano wa VETA Sitta Peter amesema kuwa VETA iko hata sekta ya Madini na baadhi ya Kampuni za Madini watashirikiana nazo. Amesema kuwa katika kwenda katika uchumi wa Viwanda kwa kazi ya VETA ni kuzalisha wajuzi wengi wa kutumika katika sekta hiyo.

Amesema kazi ya VETA licha ya kutoa mafunzo ya ufundi wamedhamiria kutatua changamoto katika jamii.
 Waziri wa Madini Dotto Biteko akiangalia ugunduzi namna sayari ya Dunia inavyokuwa na mvutano na jinsi inavyojilinda wakati alipotembelea la VETA katika Maonesho ya 43  Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar Salaam.
 Waziri wa Madini Dotto Biteko akioneshwa ngozi wanazozitumia kutengeneza viatu katika Chuo cha VETA Dakawa katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa  Madini Dotto Biteko akiangala kofia ngumu inavyofanya kazi kwa kufanya pikipiki kuwaka kwake ni mpaka dereva pikipiki avae kofia hiyo ngumu katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akipata maelezo kutoka Kwa Meneja Mawasiliano wa VETA Sitta Peter namna  ya Mfumo wa Taa za kuongozea magari iliogunduliwa katika Chuo cha VETA Kihonda katika Maonesho ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata mafunzo ya mapishi katika banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...