Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Kagera.

Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha Vijana kutoka Kagera Halima Bulembo,anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera ,ambapo ametembelea Wilaya ya Muleba na kutoa msaada wa Vitanda vya hospital,Magodoro,Mashuka na Delivery Pack katika Zahanati ya Ruhanga iliyopo Kamachumu Wilayani Muleba,

Mh Halima amesema kuwa lengo kubwa la ziara na msaada huo ni kuunga Mkono jitahada zinazofanywa na Mh Rais Magufuli ikiwa ni sambamba na kuwasaidia wagonjwa pamoja na akina mama wajawazito pindi wanapoenda kujifungua.

Licha ya changamoto chache katika sekta ya afya, Serikali ya awamu ya Tano imeboresha huduma ya Afya kwa kiwango kikubwa, kwa kuongeza vituo vya Afya, Zahanati, na ujenzi Wa Hospitali Mpya sambamba na upatikanaji wa dawa katika Vituo hivyo, huku jitihada zaidi zikielekezwa katika kuboresha huduma ya Afya ya Uzazi wa Mama na motto.

Katika ziara hiyo amemkuta mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage ambaye amepongeza Kwa msaada huo Mkubwa alioutoa huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kujitoa katika shughuli za kuchangia maendeleo hususani mambo yanayogusa jamii.
 Mbunge wa Vijana Mkoa wa Kagera, Pichani, Mhe. Halima Bulembo akikabidhi msaada wa Mashuka ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyoahidiwa katika Zahanati ya Ruhanga Kamachumu Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji Ruhanga pamoja na wanafunzi, wakiwa wanaendelea kumsikikiza Mhe. Halima Bulembo (hayupo pichani) wakati wa tukio la utoaji Vifaa vya huduma ya Afya katika Zahanati ya Ruhanga Kamachumu. 
Pichani ni Mhe. Halima Bulembo akiwa anaendelea kufuatilia moja ya shukrani kutoka kwa wakazi wa Ruhanga, pembeni ni Mhe . Charles Mwijage (MB) na Fahami Matsawili mwanaharakati wa mambo ya Kisiasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...