Na Woinde Michuzi Tv ,Arusha

Wafanyabiashara wa Nyama zaidi ya 135 katika jiji la Arusha wametishia kuanza kuziteketeza Ngozi za Mifugo wanazozalisha baada ya kuchinja Mifugo, kwa kile walichodai ni kushindwa kupata masoko ya uhakika ya zao hilo kufuatia kampuni zinazojihusisha na biashara hiyo kuwalipa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne.

Wakiongea katika kikao cha Pamoja leo,mwenyekiti wa wafanyabiashara hao wa Nyama katika jijini la Arusha ,Alex Lasike amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kukata tamaa na zao hilo kutokana na kukosekana kwa masoko ya uhakika na bei ya zao hilo ikiendelea kuporomoka.

Amesema hali hiyo imewafanya wafanyabiashara hao kutishia kuachana na biashara ya Ngozi badala yake watakuwa wakiziteketeza kwa moto au kuwapa Mbwa kama chakula baada ya kampuni ya Salex Limited na Ngozi Center za jijini Arusha ,zinazonunua bidhaa hiyo kushindwa kuwalipa mamilioni ya fedha wanazozidai katika kipindi cha miaka Minne.

"Ni mwaka wa Nne tunauza Ngozi tena kwa bei ndogo ya shilingi 100 kwa kilo katika kampuni hizo binafsi lakini hatujawahi kulipwa kwa muda mrefu na watu wanazidi kuumia " Alisema Alex

Alifafanua kwamba kila siku wafanyabiashara hao wanachinja ng'ombe,Mbuzi na Kondoo zaidi ya 150 lakini Ngozi zinazopatikana zinakusanywa na kampuni hizo kwa ajili ya malipo, lakini hadi leo wanasotea malipo yao ya zaidi ya miaka minne.

Wameiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika ili waachane na kampuni hizo zinazonunua kwa mkopo na kushindwa kuwalipa kwa wakati.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Nyama,Katika jiji la Arusha, Hopson Minja na Elius Lazaro wamesikitishwa na kampuni ya Salex na Ngozi Center zinazonunua ngozi kushindwa kuwalipa fedha zao na kuitaka serikali iingilie kati ili wapate haki zao.

"Kwa mfano Mimi nadai zaidi ya sh,million nne sijalipwa kwa zaidi ya miaka minne ,tunaiomba serikali itusaidie kupata haki zetu pamoja na kututafutia soko la uhakika la Ngozi" Alisema Minja.

Mmoja ya wamikili wa kampuni ya Ngozi ya Salex Limited ya jijini Arusha, Mahsin Ghalib amesema biashara ya soko la Ngozi duniani imeporomoka kwa kiasi kikubwa kutokana na Nchi zilizokuwa zikinunua siku hizi hazinunui kwa wingi jambo linalopelekea biashara hiyo kudorora.

"Kiwandani kwangu kuna shehena ya Ngozi zaidi ya Kilo milioni 2.8 , sina mahala pa kuuzia masoko hakuna nchi zilizokuwa zikinunua siku hizi hawataki Ngozi za chumvi" Alisema Ghalib

Ameiomba serikali imsaidie kupata mkopo wa fedha ili anunue machine zitakazomsaidia kuchakata Ngozi hapa nchini na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya Nchi.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Nyama katika jijini la Arusha ,Alex Lasike akiongea katika kikao chao  kilichofanyika leo jijini hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...