Daniel Ulimboka ni Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya teknolojia za kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.
Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho za teknolojia ya kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.


Na Vero Ignatus,Arusha.

Mbegu bora za mahindi aina ya Tumbili 419 kutoka Kampuni ya Mbegu ya Seedco ni mbegu ambazo zinahimili mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamekua yakisababisha uhaba wa mvua katika maeneo mengi nchini hivyo kumsaidia mkulima kupata mavuno mengi licha ya mabadiliko hayo. 

Daniel Ulimboka ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Seedco, akizungumza katika Maonyesho ya kilimo Teknolojia yaliyofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tari Seliani ,alisema wamefanya utafiti nana wamekuja na mbegu bora ambazo zinahimili hali ya ukame licha ya uhaba wa mvua bado zinaleta mavuno ya kutosha kwa mkulima.

"Tuna mbegu aina ya tumbili 419 ambayo inafanya vizuri sana hasa katika kipindi hiki ambacho hakuna mvua za kutosha wakulima bado wamekua wakipata mavuno na kufurahia kilimo" Alisema Daniel

Melchiory Temu Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha aliwataka watafiti kubuni teknolojia zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili wakulima waweze kupata mazao badala ya kupata hasara kutokana na mabadiliko hayo ambayo yamekua yakileta athari na kusababisha kushuka kwa uzalishaji.

Aidha aliwataka Wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuwaletea manufaa wakulima na taifa kwa ujumla.Gerald Masila ni Mkurugenzi wa Baraza la Nafaka Afrika Mashariki alisema kuwa wanafanya juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko ili waweze kupata faida ya kilimo chao na kujikwamua kiuchumi.

Yasinta Pius na Leskar Mollel ni wakulima waliofika katika maonyesho hayo Mollel wameiomba wadau kuzifikisha teknolojia hizo maeneo ya vijijini ili ziweze kuwanufaisha wakulima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...