Na Woinde Shizza  Michuzi Tv,Arusha

Mwitikio wa uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura jimbo la Arumemeru Mashariki  upo vizuri  na hasa katika Kata za  Akheri,Kwarisambu, Poli ambapo wananchi wanajitokeza kwa wingi wakiwamo vijana waliotimiza miaka 18 ambao wanaojiandikisha kwa mara ya kwanza

 Hayo yanebainishwa na Ofisa Mwandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki Emmannuel Mkongo wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mwitikio wa wananchi katika kujiandikisha kwenye daftari hilo ambapo amesisitiza kwenye kata hizo mwitikio ni mkubwa zaidi maeneo yenye mikusanyiko ya watu unaotokana na shughuli za kibiashara tofauti na maeneo ya pembezoni ambapo mwitikio ni mdogo.

Mkongo amesema hakuna changamoto iliyojitokeza ikaathiri mchakato huo hadi sasa kwani baadhi ya Mashine za BVR zilizo kuwa na itilafu na kushindwa kuchapa  vitambulisho ilitatuliwa na wataalamu wa TEHAMA .

 "Nilipopita kukagua zoezi hili la uandikishaji  Kituo cha Kupigia kura chuo cha Mifugo Tengeru LITA  nilikuta BVR KIT haifanyi kazi  na kwa sasa wataalam wa TEHAMA mameshatatua na wananchi wanapata huduma"ameeleza Mkongo.

Mkongo ametoa rai kwa  wananchi kuhifadhi vizuri vitambulisho vyao vya  Mpiga Kura  kwani wengi wao wanaokwenda kuboresha taarifa zao  imeoneka vitambulisho vyao vya awali kuharibika (vunjika) kutokana na kuvikali vikiwa mifukoni ,alibainisha  Kitambulisho cha mpiga kura ni kitambulisho muhimu kwani kinakupa haki ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais ,Mbunge na Diwani hivyo hamna budi kuvihifadhi vizuri.

Aidha Mkongo ametoa rai kwa wananchi ambao wanataka kurekebisha na  kuhamisha taarifa zao,kufuta taarifa zao, wanaotimiza umri wa  miaka 18 ifikapo  Octoba 28 mwaka 2019 na wenye miaka umri wa 18 ambao hawajajiandikisha kujitokeza na kujiandikisha na kupata vitambulisho vya Mpiga Kura kwani zoezi hilo litadumu kwa siku saba tu.
Afisa uandikishaji jimbo la Arumeru Mashariki ,ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo akifuatilia utendaji wa BVR KIT Operator Mbora Kweka ,katika kituo cha kupiga kura Mkwakirika Kata ya Poli
Ayob mbise akiweka alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...