Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Ili kuweza kuongeza kasi kubwa ya jamii kuwa na mazoea ya kutembelea makumbusho na kujionea mambo ya kale sekta ya elimu imeshauriwa kujenga msingi mzuri kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa masomo yanayohusiana na mambo ya kale 

Wito huo umetolewa na afisa elimu wa makumbusho ya azimio la Arusha Mkoani Arusha Godfrey Emanuel wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya umuhimu wa kutembelea makumbusho

Aidha amesema kuwa, jamii imekuwa ikisahau kwenda kujifunza mambo ya kale na kuwaachia wanafunzi jambo linalosababisha kushindwa kufanya ubunifu wa mambo mbalimbali kupitia mambo ya kale

Kwa upande wake mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha Costantine Misago amesema kuwa kupitia sheria mbalimbali za makumbusho jamii inapaswa kutembelea bila kizuizi chochote na kukaribisha wageni kutoka mataifa mbalimbali kujionea historia mbalimbali zilizofanywa na watu wa kale

Alibainisha kuwa kunamambo mengi ya kale yanapatikana katika makumbusho yetu hivyo ni muhimu wanafunzi wananchi kutembelea makumbusho haya na kujionea mambo mbalimbali yaliofanywa zamani pamoja na yaliogunduliwa na wanasanyansi pamoja na historia mbalimbali za watu wakale

Alisema kuwa kutembelea makumbusho hizi pia zitasaidia kuongezea mapato ,pia aliwasihi wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza makumbusho mbalimbali zilizopo nchini nakuwahamasisha wananchi kuwa natabia ya kutembelea wananchi hao 

Makumbusho iliopo jijini Arusha ipo kwenye boma lililojegwa na wajerumani miaka ya 1900 iliokuwa ikitumika kama jengo la utawala na mawasiliano wakati wa ukoloni wa kijerumani na makumbusho haya yalifunguliwa rasmi mnamo mwaka 1987 na kuonyesha historia ya binadamu wa kale ,ikiwepo pamoja na tafiti zilizofanywa katika tafiti zilizofanywa katika bonde maarufu la Olduvai na alama za miguu wa binadamu wa kale za Lawtoli .

Aidha makumbusho haya inafanya maonyesho juu ya entomolojia ambayo huwasilisha baadhi ya wadudu ,ndege,na wanyama pamoja na umuhimu wao kiuchumi ambapo pia ni kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea makumbusho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...