Mkurugenzi wa kapuni ya Motisun Group Pawan Patel (wa pili kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania Inviolata Itatiro kwa ajili yakusaidia maandalizi ya timu ya Taifa itakayoshiriki mashindano ya kuogelea ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Gwangju, Korea Kusini.Kulia ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sayona Drinks Nitin Menon na kushoto ni Maneja wa Masoko Erhard Mlyansi 
……………….. 
Na Mwandishi wetu 
Dar es Salaam. Waogeleaji wa Tanzania wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Korea Kusini kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Dunia. 
Safari hiyo itajumuisha waogeleaji wanne, Hilal Hemed Hilal, Collins Saliboko ambao watashindana kwa upande wa wanaume na Sylvia Caloiaro na Shivan Bhatt ambao watashindana kwa upande wa wanawake. 

Hilal na Collins watasafari mpaka Dubai na kukutana na waogeleaji wa kike, Sylvia Caloiaro na Shivan Bhatt ambao walikuwa wanafanya kambi ya mazoezi hapa nchini chini ya kocha Alex Mwaipasi na Michael Livingstone. 
Waogeleaji hao wapo morali ya juu baada ya kampuni ya Motisun Group kukabidhi mchango wao wa dola za kimarekani 2,000 (Sh 5 million) ili ziwasaidie katika mahitaji mbalimbali ya mashindano hayo. 

Meneja Mkuu wa kampuni ya Sayona Drinks Limited, Nitin Menon alikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA), Inviolata Itatiro na kuwaomba waogeleaji hao kupambana vilivyo kwa ajili ya Taifa. 

Menon alisema kuwa waogeleaji hao wanatakiwa kutambua kuwa Watanzania zaidi ya milioni 45 wanasubiri kuona matokeo mazuri kutoka kwao pamoja na ugumu wa mashindano. 

Alisema kuwa Motisun Group inajisikia fahari kubwa kuwa mdau wa michezo na kuahidi kuendelea kufanya hivyo nchini. “Naomba mkafanya vizuri katika mshindano haya na kuendelea kuleta hamasa kwa wanamichezo nchini, tupo pamoja nanyi katika kuendeleza gurudumu la maendeleo ya michezo nchini,” alisema Menon. 

Alisema kuwa hiyo si mara yao ya kwanza kusaidia michezo kwani waliweza kusaidia kambi ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na mashindano ya Afcon na pia kusaidia fainali za vijana wa chini ya miaka 17 za Afcon zilizofanyika hapa nchini. 

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro aliipongeza kampuni hiyo na kuziomba kampuni nyingine kusaidia mchezo huo. “Ni fahari kwetu kuona Motisun Group imefungua njia. Bado tunahitaji msaada kutoka kwa wadau ili kufanikisha zoezi zima la kuwasafirisha waogeleaji wetu kwenda Korea,” alisema Inviolata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...