Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Watanzania wametakiwa kuendelea kuthamini na kuzienzi mila ,desturi na tamaduni zilizopo katika jamii ili kuendelea kuziridhisha kwa vizazi na vizazi ili zisisahaulike .

Hayo yalisemwa jana na Afisa utamaduni wa mkoa wa Arusha,Irene Ngao wakati akizungumza katika siku ya tamasha la Kanono la wanaumoja wenye asili ya Karagwe na Kyelwa mkoa wa Kagera waishio Arusha.

Ngao alisema kuwa,serikali inatambua uwepo wa mila na desturi mbalimbali zilizopo katika jamii ,hivyo wanategemea ziridhishwe zaidi kwa vizazi vyetu vilivyopo na vinavyokuja ili wao waendeleze na utaratibu huo ili zisahaulike katika jamii.

"nasisitiza kila kabila liendee kuenzi tamaduni na mila zao na tuhakikishe zinatuunganisha badala ya kutogombanisha kwani serikali nayo kwa upande wake inaendelea kufundisha somo la utamaduni mashuleni ili kuhakikisha watoto wetu wanazitambua mila na desturi zilizopo ."alisema Ngao.

Naye Mwenyekiti wa umoja huo ,Wilibald Ngambeki alisema kuwa,wamekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha hilo kila mwaka ambapo hili ni tamasha la 23 kufanyika hapa mkoani Arusha.

Alisema kuwa,lengo la kufanya tamasha hilo ni kuhakikisha watoto wanaozaliwa mjini wanazijua mila na desturi zao na kuhakikisha hazipotei .

Ngambeki alisema kuwa,kila mwaka wamekuwa wakikutana na kuonyesha tamaduni zinazofanywa na jamii hizo na kuwapa fursa watoto wao kujionea maswala mbalimbali na kujifunza ambapo kupitia tamasha hilo wataendelea kuwaridhisha watoto wao mila hizo.

"kwa kweli utamaduni ni kitu muhimu sana kwani zinasaidia sana kupunguza makali ya utandawazi badala yake jamii kuendelea kujikita katika tamaduni zao na kuacha kuiga mambo ya utandawazi ,hivyo nashauri kila kabila liendelee kuenzi ili zisipotee."alisema .

Naye mmoja wa wanachama katika umoja huo,Albert Kakulima alisema kuwa,wamekuwa wakikutana kwa lengo la kutunza mila , desturi na tamaduni zao ili zisipotee kwani asilimia kubwa ya watoto waliozaliwa huku mjini hawazijui na bila kufanya hivyo hawatazitambua na badala yake zitaendelea kupotea.

Aidha aliyataka makabila mengine kuendelea kuenzi tamaduni zao kwa kukutana mara kwa mara kwani bila kufanya hivyo zinaendelea kupotea na itabaki historia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...