Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi wa Wizara hiyo.

Bw. James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi  wote wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.

Aidha Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Bajeti hiyo.

Kwa upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.

Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Fedha na Mipango  Bw. Doto James, akifungua kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma, Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akifafanua jambo wakati wa kikao Kati ya Viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma, ambapo Watumishi waliaswa  kufanya kazi kwa bidii na weledi.
 Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila akijibu hoja katika kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara  ya Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Mgonya Benedicto akichangia hoja wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Alfred Dede akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Umma (TUGHE) wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenjel James akichangia mada katika kikao cha viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo ambapo Watumishi walitakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Fedha na Mipango  Bw. Doto James, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu kikao cha viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo, kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
Mtumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Hilder Rugemalira akitoa hoja wakati wa kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...