Kuelekea Kilele cha Wiki ya wananchi Agosti 4 2019, Uongozi wa Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Kariobangi Sharks kutoka Nchini Kenya.
Mchezo huo maalumu unatarajiwa kupigwa kwenye kilele cha Siku ya Mwananchi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Makamu Mwenyekiti - Fredrick Mwakalebela amesema Wiki ya Mwananchi itaanza Julai 27 na kufanyika kwa uzinduzi ambapo itafanyika matukio mbalimbali ikiwemo kufanya shughuli mbalimbali za Kijamii pamoja na kuitangaza siku hiyo sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
Mwakalebela amesema, wanacheza na Kariobang baada ya AS Vita ya DR Congo kuomba udhuru ya kuingiliwa na ratiba ya CAF baada ya kupokea barua hiyo wakafanya mazungumzo na Kariobang na kukubali kuja nchini kucheza mchezo huo wa kirafiki.
Kwa upande wa katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki hiyo ya Mwananchi, Deo Mutta alisema kuwa "Uzinduzi ya Wiki ya Mwananchi itaanza rasmi Julai 27, mwaka huu kwa baadhi ya wanachama wa Yanga kwenda Zanzibar kutembelea kaburi ya muhasisi wa Yanga, Abeid Amani Karume na baada ya hapo jioni tutacheza mchezo wa kirafiki wa wanachama.
Mutta ameeleza watarejea Dar siku inayofuata na kuanza kukusanya kijiji kwa kuanza kutembea na gari kubwa la wazi la GSM litakalokuwa na wasanii wa muziki na filamu.
"Gari hilo la wazi litaanzia safari zake Kutoka Makao Makuu ya Klabu na kupita Morocco, Mwenge, Bunju, Bagamoyo, Kiwangwa, Msata, Lugoba, Msoga na Mdaula na baadaye kwenda Morogoro na kurejea tena kwa kupitia njia ya Kimara naMbezi," alisema Mutta.
Awali Yanga walipanga kuadhimisha wiki ya mwananchi Julai 27 kutokana na muingiliano wa ratiba ya michuano ya kufuzu CHAN kati ya Tanzania na Kenya Julai 28 ratiba kubadilishwa na kuelekea Agosti 4 mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredirick Mwakalebela akitoa taarifa ya kubadilika kwa timu watakayocheza nayo mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4 mwaka huu baada ya timu ya awali As Vita kuomba udhuru kutokana na ratiba ya michuano ya kimataifa ya CAF iliyotoka mapema wiki hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...