Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, kwa ajili yakutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadayekuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakipata
maelezo kutoka kwa kiongozi wao Prof.Li Kunruonan, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, wataalam hao wako nchini kwa siki 11 kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadaye kuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
Baadhi ya Wataalam kutuka kampuni ya Baidu kutoka China wakicheza
ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
Wacheza ngoma wa Kikundi cha Nimujo wakitoa burudani kwa wageni wa
kampuni ya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
Mpiga ngoma wa Kikundi cha Nimujo akipiga ngoma kwa wageni wa kampuniya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege waKimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.

********************

Na. Paschal Dotto-MAELEZO
22-08-2019

Katika Jitihada za kukuza utalii nchini Taasisi iliyopewa jukumu hilo yaani Bodi yaUtalii Tanzania(TTB) ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Nchini China, wamewezesha kampuni ya Beijing Pseacher Business na Baidu kuja nchini kutembelea na badaye kufanya kazi ya uzalishaji wa picha mjongeo(Film) na picha zitakazowekwa kwenye mtando wao wenye wafuasi takribani 700 kwa lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alisema kuwa ujio wa wageni kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii, kwani utawezesha kuwepo kwa mradi mkubwa wa kupiga picha na kutengeneza Film ya vivutio vya utalii Tanzania ambavyo vitatangazwa kwenye mtandao wa Baidu na kuwezesha watalii kutoka China kuja kutalii nchini.

“Tumefanya kazi kubwa kwa kushirikiano na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China, ambapo tumepata kampuni hii waliowasili leo kutembelea na baadae kuja kufanya mradi wa kupiga picha, kutengeneza makala ya vivutio vyetu, vyakula vyetu vya asili, lakini pia watapata fursa ya kutembelea Serengeti, Bonde la Mamlaka ya Ngorongoro, Zanzibar na bagamoyo na badae watafanya mradi huo ambao utaisaidia Tanzania kuliteka soko la utalii la China”, Geofrey Tengeneza.

Tengeneza alisema kuwa wataalam hao 12 kutoka Baidu wamekuja kwa lengo la kuona jinsi gani watafanya mradi huo mkubwa ili kuwezesha uzalishwaji Film, picha za kawaida na kuziweka kwenye mtandao wao ambao unawafuasi wengi na hii itasaidia kukuza soko la utalii wa Tanzania kwa upande wa soko la China.

Aliongeza kuwa leongo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka china na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradi huo wa kampuni ya Baidu.

Kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo, Prof. Li Kunrounan alisema kuwa wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo wa uzalishaji wa film kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa ili kukuza ushirikiano wa Tanzania na China kwenye Sekta ya Utalii.

“tumekuja kujionea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini Tanzania na baada ya hapo tutakuja sasa kufanya film na picha ambazo tutaziweka kwenye mtandao wetu unafuatiliwa na watu zaidi ya milioni 700 nchini China”; alisema Prof. Li Kunrounan.

Prof. Li Kunrounan alieleza kuwa Tanzania ina vivutio vingi sana ikiwemo wanyama, mabonde pamoja na fukwe mbaliambali hayo ni moja ya maeneo ambayo yanahitaji kuitangazwa, lakini pia watu wake ni wakarimu sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...