Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (kushoto) akiangalia chungu kilichotengenezwa na wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha zaidi kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania kwa kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mpango huo umeonesha matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya watanzania kiuchumi.
Wanawake wajasiriamali waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, wakiwa na bidhaa za Shanga wakizionesha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (hayupo pichani), katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (kushoto) akiangalia chungu kilichotengenezwa na wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
Wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam, wakishangilia baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (hayupo pichani) kuahidi Benki yake kuongeza fedha katika mpango huo, alipotembelea utekelezaji wake.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Keko Machungwa, Bw. Uwesu Misanga, akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (hayupo pichani), alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, na wadau wengine wa maendeleo alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa mpango huo, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

******************

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha zaidi kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania kwa kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mpango huo umeonesha matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya watanzania kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 zilizopo Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wakati alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa TASAF awamu ya kwanza na ya Pili katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa ameshuhudia mwenyewe wanawake wakiwa wamezalisha bidhaa mbalimbali vikiwemo viatu, vikapu, shanga, mikoba, vyungu, urembo na nguozilizotengenezwa kupitia mpango wa TASAF, jambo linalodhihilisha manufaa yampango huo kwa Kaya masikini katika kukuza uchumi wao.

“Kwa kuwa nawakilisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika Benki ya Dunia,Washngton Marekani, nimejionea kwa macho yangu bidhaa mbalimbalizilizotengenezwa hasa na wanawake, hivyo naenda kupeleka ujumbe huo muhimu ili Benki iweze kuongeza fedha zaidi kwa awamu zingine kwa ajili ya mpango huu wa TASAF kutokana na manufaa yake katika kupunguza umasikini nchini Tanzania”, alieleza Bi. Kabagambe.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Keko Machungwa, Bw. UwessuMisanga, alisema kuwa kuanzia mwaka 2015 hadi Februari, 2019, fedha walizolipwa walengwa wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo lake ni takribani Sh. milioni 86.1.

Alisema manufaa ya mpango huo ni pamoja na upatikanaji wa mahitaji muhimu kama Chakula, kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni na kuhudhuria Kliniki kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka Kaya Masikini.

Mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa kipato kwa walengwa kutokana na biashara ndogondogo zinazofanywa na kaya hizo lakini pia kuboreshwa kwa mahitaji muhimu ya wanafunzi kutokana na ruzuku.

Aidha Bw. Misanga, alibainisha changamoto za utekelezaji wa Mpango wa TASAFkuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, baadhi ya Kaya kukosa fursa ya kuingia kwenye mpango, uhaba wa maeneo ya kufanyia shughuli za kuongeza kipato na pia uhaba wa mitaji katika vikundi vya wajasiriamali vilivyoanzishwa na Kaya hizo.

Alisema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali inafanya tathmini namapitio ya mpango kwa awamu ya kwanza ili kuwezesha Kaya zilizoachwa kuingizwa katika mpango huo na pia Ofisi ya Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam, imewaelekeza wanakikundi wa ujasiriamali kuwasilisha mahitaji ya eneo kwa kuzingatia shughuli wanazotaka kufanya ili kutatua changamoto zao.

Baadhi ya wanufaika wa TASAF waliotoa shuhuda zao mbele ya Mkurugenzi huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwawezesha kujikwamua kimaisha na pia wameomba kuendelezwa kwa mpango huo kwa kuwahusisha watu wengi zaidi na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...