Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally akizungumza na viongozi wa CCM na wananchi katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya viongozi wilayani Meatu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa saamu kwa niaba ya wananchi, katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Kutoka Kulia Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani wakiwa katika Daraja la mto Sibiti.
Sehemu ya Daraja la Mto Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akipewa maelezo na viongozi wa Chama na Serikali wilayani Meatu na Mkoani Simiyu wakati alipotembelea daraja la Sibiti mara baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.

*************



Na Stella Kalinga, Simiyu

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally ametoa salamu za rambirambi na kuwaombea majeruhi na waliofariki katika ajali ya moto Mkoani Morogoro, huku akitoa wito kwa wananchi kuwa zinapotokea ajali wawe wepesi wa kuokoa watu na mali za waliopata ajali badala ya kukimbilia kuchukua vitu ili kuepusha madhara.

Dkt. Bashiru ametoa salamu hizo wakati akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Meatu katika kikao cha Ndani kilichofanyika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Agosti 11, 2019 ambapo amewaombea marehemu wote wapumzike kwa amani na majeruhi wapate afya njema ili waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.

“Natoa pole kufuatia vifo vya wenzetu waliofariki katika ajali ya moto kule Mkoani Morogoro tuendelee kuwaombea waliotangulia mbele ya haki wapumzike kwa amani na wale majeruhi waweze kupata afya na kurejea katika shughuli za kujenga Taifa”

“Kama Mwenyekiti wetu na Rais wetu alivyosema, tunapopata majanga kama haya ya ajali ni vizuri wote tuwe wepesi wa kuokoa waliopata ajali na mali badala ya kukimbilia kuchukua vitu kuepusha madhara makubwa” alisema Dkt. Bashiru.

Akizungumza na Viongozi wa CCM wilayani Meatu, Dkt. Bashiru amewataka viongozi hao kutoa taarifa za watu wanao nunua pamba kwa njia ya Umachinga, pasipo kutumia utaratibu unaotakiwa wa kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na ujenzi huku akiwashukuru wabunge wa wilaya ya Meatu(Jimbo la Kisesa na Jimbo la Meatu) kwa namna wanavyojitoa binafsi na kupitia mifuko ya majimbo kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Magufuli kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Draja la Sibiti ambalo ujenzi wake umerahisisha mawasiliano na utachangia katika kukua kwa uchumi wa wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.

Mara baada ya kuhitimisha kikao cha ndani na viongozi wa CCM Wilaya ya Meatu, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally alipata fursa ya kutembelea na kuona ujenzi wa Daraja la Sibiti ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo alipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo linaiunganisha mikoa ya Simiyu na Singida.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amesema kutokana na ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti Halmashauri ina mpango wa kupanua stendi ya Mjini Mwanhuzi kwa kuwa magari mengi yameanza kupita Meatu kupitia daraja hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...