Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filam hapa nchini. Kushoto ni Afisa Utamaduni wa bodi ya filamu nchini, Clerence cheles.
Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filam Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akionesha waandishi wa habari  filamu ambazo zimekamatwa mtaani kwa kutokusajiliwa katika bodi ya filam nchini na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filamuhapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Idara ya utawala bodi ya Filamu nchini, Abdallah Amanzi.
Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filam Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filam hapa nchini.Kushoto ni Afisa Utamaduni wa bodi ya filamu nchini, Clerence cheles.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
FILAMU kumi zimekamatwa zikiwa sokoni huku zikiwa hazijapitia hatua mbalimbali zikiwemo ukaguzi wa miswada ya filamu hizo pamoja na uhakiki wa filamu hizo baada ya kutengenezwa na kutokuwa na daraja maalumu linaoonesha rika husika la kuangalia filamu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kaimu katibu mkuu wa bodi ya filamu nchini Dkt. Kiagi Kilonzo amesema kuwa filamu hizo zimekamatwa zikiuzwa kinyume na taratibu.

"Ili filamu iingie sokoni lazima zipitie hatua mbalimbali, ikiwemo kuleta muswada katika bodi ya filamu ili uweze kupitiwa, uhakiki baada ya kutengenezwa kwa filamu husika ili iweze kupangiwa daraja maalumu la rika la kuangalia kutokana na maudhui ya filamu husika" ameeleza Dkt. Kilonzo.

Amesema kuwa baada ya filamu hizo kukamatwa wahusika wameitwa kwa maridhiano zaidi huku akieleza kuwa kuna filamu nyingi zinazouzwa kinyemela na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka ikiwemo kulipa faini na kifungo. 

"Kifungu cha 20 cha kanuni inayosimamia masuala ya filamu inafafanua kuwa mtu yeyote anayetengeneza picha jongefu nchini kwa maonesho ya hadhara lazima akabidhi kwa bodi ya filamu hiyo ili iweze kupitiwa na kupangiwa daraja na yeyote atakayekiuka sheria na kanuni zilizopangwa atapambana na mkono wa sheria ambapo mzalishaji, msambazaji na muuzaji atakayekwenda na  kinyume cha sheria atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa kila kosa na akikaidi atapelekwa mahakamani ambako akishindwa kesi atalipa faini ya shilingi milioni tano, au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja" ameeleza.

Vilevile amesema kuwa mafunzo na elimu yanaendelea kutolewa kwa wauzaji, wasambazaji, wazalishaji na wasanii katika maeneo mbalimbali ili waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria zilizowekwa.

Filamu zilizokamatwa katika msako huo Ni pamoja na Mbwiga, Unaibiwa, Mwanaume wa Dar, Chumba cha kati, Jadu, Adui, Ndumba, Mama Kisheti,  Tukutane Dar na Sarah Dikonko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...