Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo leo hii Agoust 16 amemaliza mgogoro wa wanafunzi uliokuwa umeota sura mbaya ya kuhatarisha hali ya amani shuleni hapo ambapo mgogoro huo ulianza tangu Augost 10 mwaka huu. Waziri huyo wa TAMISEMI alitoa onyo kwa walimu ambao inaonekana wameshindwa majukumu yao ya kiuongozi hadi shule kuingia katika mapigano makubwa kati ya kidato cha tano na kidato cha sita pamoja na kuchipuka kwa tofauti za mitazamo ya kidini shuleni hapo.

Wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamemshukuru sana waziri huyo kwani walikiri kwamba uhasama shuleni hapo ulikuwa mkubwa sana.

Waziri huyo alifanikiwa kuongea na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa pamoja na kamati ya Wilaya ya Moshi,Bodi ya shule wakiwa pamoja na walimu wote wa shule hiyo, na kuhitimisha na kikao cha wanafunzi.
Jafo alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Ngwila kuendelea kufanya uchunguzi wa waanzilishi wa chokochoko hizo ili watakao bainika wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Aidha,Jafo alimaliza ziara hiyo shuleni hapo kwa kuunda timu kumi zenye mchanganyiko mbalimbali ambazo zitashindana katika michezo mbalimbali na kuzipa majina ya Tanzanite,Gold,Diamond,Kilimanjaro, Manyara,Serengeti,Ngorongoro,Mikumi, Nyerere Park, na Ruaha kitendo ambacho kilisababisha shangwe kubwa kwa wanafunzi hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...