Uchambuzi Wa Habari: 

Mambosasa Sasa Awape Fursa Walemavu Kwenye Sadc

Ndugu , 

Marufuku ya bodaboda kuingia mjini wakati huu wa mkutano wa Sadc ni sahihi. Hoja za Kamanda Mambosasa ni za msingi. 

Hata hivyo, leo nilipata nafasi ya kufika pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwenye maonyesho ya Sadc. 

Ushauri wangu:

Ili kuvutia watembeleaji wengi zaidi wa maonyesho ya Sadc yanayoendelea sasa kunahitajika usafiri wa haraka na wa gharama nafuu kufika na kutoka eneo la tukio pale Mwalimu Nyerere Conference Centre.

Marufuku ya bodaboda sawa, lakini, Kamanda Mambosasa na waandaaji wa tukio wangetoa fursa ya ajira kwa walemavu waendesha bajaj ili kuwasaidia watembeleaji kwenda na kutoka eneo la tukio.

Ingewezekana kabisa, kukaandaliwa utaratibu wa kuwepo kwa bajaji  50 za walemavu. 25 zikawapo nje ya eneo la tukio zikiwa na stika za usajili za Sadc zenye namba na jina la dereva, na 25 nyingine zikawepo pale Posta Mpya kwa utaratibu huo huo . 

Waendesha bajaj hao walemavu wapewe na waandaaji hata elfu 20 kwa siku kila mmoja na wawatoze kila abiria shilingi mia tano kwa safari moja ya kwenda kwenye eneo la tukio na kurudi Posta Mpya. Bajaj moja inabeba abiria watatu mpaka wanne.

Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeongeza idadi ya watembeleaji na wakati huo huo kutoa fursa kwa walemavu wetu waendesha bajaj kujiongezea kipato kipindi hiki cha maonyesho ya Sadc na mkutano wa Sadc hapa nchini mwetu.

Ni ushauri tu.

Maggid Mjengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...