MKUU wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wawekezaji wa viwanda kuhakikisha wanazingatia haki za wafanyakazi kwa kuwalipa maslahi yao kama inavyotakiwa bila la kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wowote kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zote za nchi kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya uwekaji wa mawe ya msingi katika kiwanda vitatu tofauti vya kuzalishia nondo,chuma pamoja na mitungi ya gesi vilivyopo Wilayani Kibaha,ambapo pia akusita kuwaasa watumishi na viongozi kuachana na vitendo vya urasimu kwa wawekezaji na badala yake watoe ushirikiano wa kutosha bila vikwazo vyovyote kwa lengo la kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.

“Kwa sasa Mkoa wetu wa Pwani tunaendelea na kutekeleza agizo la Rais wetu Dk. John Pombe Maguli katika ujenzi wa viwanda mbali mbali, hivyo kitu kikubwa ninachowaomba wawekezaji wote wanaokuja kuhakikisha wanazingatia haki za wafanyakazi ili kuweza kutimiza malengo ambayo yamewekwa na serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,”alisema Ndikilo.

Aidha katika hatua nyingine alibainisha kuwa wawekezaji ni chanchu kubwa ya kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi kutokana na wengine wao kuweza kupata fursa mbali mbali za ajira pindi viwanda vinapoanzishwa hivyo ni jukumu la watendaji na viongozi kuwa bega kwa bega na wadau wa maendeleo ili kuweza kuongeza zaidi ujenzi wa viwanda vingine.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya lake group Ally Awadhi lengo lao kubwa ni kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa viwanda pamoja na kuwainua wananchi kiuchumi hasa ambao wanaoishi katika kaya ambazo ni masikini kuwapatia fursa za ajira.

Pia aliongeza kwamba kutokana na kuwepo kwa uwekezaji wa viwanda hivyo kutasaidia kuwainua wananchi wa Wilayani Kibaha pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kutokana na kupata ajira ambazo zitasaidia kuwaongezea kipato sambamba na kuchangia katika ulipaji wa kodi amabazo zitafanya pato la Taifa kuongezeka.

Nao baadhi ya wafanyakazi katika viwanda hivyo walimpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kwa kuwa na sera ya ujenzi wa viwanda katika maeneo mbali mbali ambavyo wamedai vimewasaidia kupata fursa ya ajira, na kuondokana na wimbi la umasikini na kumwomba mwekezaji huyo kuwaongezea ujira kulingana na kazi wanazozifanya.

KUKAMILIKA kwa viwanda hivyo vitatu vya utengenezaji wa nondo,na chuma hususan cha kutengenezea mitungi ya gesi kutaweza kusaidia wananchi kwa kiasi kikubwa fursa za ajira pamoja na kupunguza changamoto ya ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kupata nishati ya mkaa ambayo imekuwa ni kero ya siku nyingi katika maeneo ya Mkoa wa Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kulia wakipongezana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Lake Group Ally Awadhi maara baada ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu tofauti vya kutengenezea nondo,chuma, pamoja na kiwanda cha kutengenezea mitundi ya gesi katika kata ya visiga Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kushoka akipata maelekezo na mmoja wa wataalamu wa kiwanda cha kutengenezea nondo na chuma, mara baada alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno.(PICHA NA VICTOR MASANGU.
  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia akipeana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni wa Lake Group mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uwekaji wa mawe ya msingi katika viwanda vitatu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani wa kulia Mhandisi Evarist Ndikilo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kati kati,pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Lake group Ally Awadhi wakiopiga makofi kwa pamoja ikiwa ni ishara  furaja mara baada ya kukamilika kwa uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalishia Nondo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa anafafanua jambo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka jiwe la msingi katika kiwanda   cha kutengenezea mitungi ya gesi ambacho kinatarajia kukamilika mwishoni mwa octoba  mwaka huu
Mkurugenzi mtendaji wa  kampuni ya Like group Ally Awadhi kushoto  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumptem Mshama wa akifuatiwwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kumaliza kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitatu vya kutengenezea Nondo, chuma pamoja na mitungi ya Gesi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...