Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amewataka mashabiki wa mpira wa miguu nchini kuacha kuangalia kwenye Televisheni bali wakajaze Uwanja.

Hayo ameyasema wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kariobang Sharks.

Ambapo katika mchezo huo Mwakyembe ameweza kupokea zawadi ya jezi ya Yanga kutoka kwa Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla kwa ajili ya Rais Dkt Magufuli kama kiashiria cha ushiriki wake kwenye michezo nchini.

Mwakyembe amesema kuwa sasa hivi ni muda wa mashabiki kwenda kujaza viwanja vya mpira pale timu zao zinapokuwa zinacheza na kuacha kuangalia kwenye Televisheni.

Amesema, mashabiki wanapojitokeza kwa wingi timu uwanjani inapata hamasa kuwa na hata mapato kwa timu yanakuwa yanapatikana kwa wingi.

Ametoa salamu kwa wana Yanga wote kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwatakia mchezo mwema pamoja anawapenda wote.
 Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla akimkabidhi jezi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe zawadi ya jezi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kama kiashiria cha ushiriki wake kwenye michezo wakati wa Kilele cha Wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mechi ya Kirafiki kati ya Yanga na Kariobang Sharks uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1 leo kwenye Uwanja wa Taifa







Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na mashabiki  na wanachama wa Yanga waliojitokeza kushuhudia Kilele cha Wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Kariobang Sharks uliomalizika kwa sare ya 1-1 mchezo uliochezwa kwenye Dimba la Uwanja wa Taifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...