Mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania kutoka Karatu Mkoani
Arusha Bi Tarsila John akitoa maelekezo kwa mteja wake ya namna ya kutumia Mifuko
y kuhifadhia Nafaka na Dawa za kuhifadhia nafaka, Bi Tarsila yuko katika
maonyesho ya NaneNane kuelezea ubora wa
mifuko hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa wauza pembejeo wilayani kilombero
mkoani morogoro ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw John Bosco
Zakaria Mvunjapori akitoa maelezo kuhusu
pembejeo za kilimo.
Mkazi wa Pawaga Mkaoni Iringa Bw. Twalibu Ubwa akifafanua
jambo kwa wateja wake kuhusu bidhaa ya mchele, Ubwa ni mwanachama wa Baraza la
Kilimo Tanzania na yuko katika maonyesho hayo kuelezea namna wanavyoshiriki
katika uongezaji thamani katika zao la Mpunga.
Muonekano wa Banda la Baraza la Kilimo Tanzania katika Viwanja
vya Mwl. Julias Nyerere Mkaoni Morogoro, ambapo Baraza limekuwa likishiriki
kila mwaka maonyesho ya wakulima NaneNane, Fika katika banda lao ili uweze
kupata taarifa sahihi kuhusu sekta ya Kilimo na mchango wake katika uchumi wanchi.
Bi Zaibab Mahenge kutoka Mafinga akiwa katika Banda la Baraza
la Kilimo Tanzania akifafanua jambo kwa mteja wake aliyetaka kujua zaidi kuhusu
bidhaa ya unga wa lishe inayozalishwa na Bi zainab ambayo inamchanganyo wa Unga
wa Dona,Soya, Mbegu za Maboga, Ulezi na Mchele.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...