Katibu Mtendaji wa
Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akifafanua jambo kwenye mdahalo kuhusu
ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye sekta mbalimbali nchini
(local content) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 08 Agosti, 2019.
Sehemu ya wajumbe wa
mdahalo huo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Katibu Mtendaji wa
Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).
Kutoka kushoto Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Tafiti za
Kimkakati kutoka Taasisi ya REPOA, Dk. Jamal Msami na Mhadhiri kutoka Chuo
Kikuu cha Mzumbe –Tawi la Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi wakifuatilia
maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa. (hayupo pichani)
Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa akifafanua
jambo katika kikao hicho.
Leo tarehe 08 Agosti,
2019 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ameongoza
mdahalo kuhusu ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye sekta
mbalimbali nchini (local content) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya
viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) yanayofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mdahalo huo
ulishirikisha pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe –Tawi la
Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi na Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati kutoka
Taasisi ya REPOA, Dk. Jamal Msami
Waliohudhuria katika
mdahalo huo walikuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya
Madini, Augustine Ollal, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume
ya Madini, Dk. Abdulrahman Mwanga, watendaji kutoka Wizara ya Madini na Tume ya
Madini pamoja na wadau kutoka taasisi za fedha na wajasiriamali.
Awali akielezea
manufaa ya ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye shughuli za
madini na sekta nyingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa alisema kuwa ni pamoja na kuinua uchumi
kuanzia katika ngazi ya chini na Taifa kwa ujumla.
Akielezea mafanikio
ya utekelezaji wa mpango wa ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma
kwenye shughuli zinazofanywa na wawekezaji nchini, Beng’l alisema wawekezaji
kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo wameanza kutumia huduma zinazotolewa na
watanzania hivyo kuongeza kipato.Alitaja miradi hiyo
kuwa ni pamoja na ule wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi
Morogoro, miundombinu, sekta ya madini na gesi.
Mapendekezo
yaliyowasilishwa na wachangiaji mbalimbali kupitia mdahalo huo yalikuwa ni
pamoja na utoaji wa elimu kwa watoaji huduma wa ndani kuhusu namna bora ya
kutoa huduma na bidhaa bora, wazalishaji na watoa huduma wa ndani kuingia ubia
na kampuni nyingine kubwa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi
na kupata uzoefu zaidi.
Akihitimisha mdahalo
huo, Profesa Manya aliwataka wadau kutumia changamoto mbalimbali kwenye sekta mbalimbali
kama fursa hususan kwenye utoaji wa huduma na kujipatia kipato.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...